August 6, 2020

IMEELEZWA kuwa jumla ya makocha 60 wamewasilisha CV za maombi ya kuifundisha Yanga katika msimu ujao wa 2020/21 ili kubeba mikoba ya Luc Eymael ambaye alifutwa kazi Julai 27 baada ya kueneza taarifa ambazo zilikuwa zinaviashiria vya ubaguzi wa rangi jambo ambalo linapigwa vita na familia ya michezo duniani kote.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha mwingine na wanaotajwa kuingia rada za Yanga ni pamoja na Hans Pluijm, Ernie Brandits, Patric Aussems, Mecky Maxime na Hitimana Thiery.

Habari zinaeleza kuwa bado uongozi wa Yanga unaendelea kupokea CV za makocha kutoka ndani ya nchi na nje ya nchi ili kuweza kukinoa kikosi hicho.

"Ndani ya wiki mbili hizi kocha mkuu mpya wa Yanga atajulikana baada ya kumfukuza Eymael hivi sasa uongozi unapitia CV za makocha mbalimbali waliotuma maombi kuja kuifundisha timu," ilieleza taarifa hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Simon Patrick hivi karibuni alisema kuwa:"Tutahakikisha tunafanya uamuzi sahihi kwa kuteua kocha atakayetufaa kutokana na ukubwa wa Klabu ya Yanga, ".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic