SHELDA Boniphace mshambuliaji wa Yanga Princess msimu wa 2019/21 ameibukia ndani ya watani zao wa jadi Simba Quuens.
Akiwa ndani ya Yanga Princess kwa msimu wa 2019/20 alitupia jumla ya mabao 11 ndani ya Ligi ya Wanawake jambo lililowafanya Simba wakavutiwa na uwezo wake.
Kocha Mkuu Simba Queens, Mussa Mgosi amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuendelea kuwa bora na kuleta ushindani Afrika Mashariki na Kati.
"Tupo imara katika maboresho yetu na kikosi chetu kimeonekana kwa msimu uliopita ambapo tumeweza kutwaa ubingwa tukiwa na mechi mkononi, bado tunahitaji kuendelea kutwaa mataji hivyo tunaboresha kikosi ili kuwa imara zaidi," amesema.








Safi Safi sana kocha mgosi mwendelezo ndo jadi yetu. Mwendo wa mataji tu.
ReplyDeleteHata wanawake wanatukimbia, Jee tunaelekea wapi au pia twende Fifa?
ReplyDeleteAlikuwa ameongeza mkataba wa miaka miwili na Yanga, sasa sijui kwa nini Simba wamemsajili
ReplyDeletehuyo mchezaji ana mkataba wa miaka miwili na Yanga TFF yote ni simba, sisi utopolo hataukubali tunaenda FIFA
ReplyDeleteKweli Team ya Kiswahili ,unajua uswahilini mtu akila nyama(mboga)anataka majirani wajue ,Sasa wapendwa sisi tuna nyama ya kitimoto(Senzo)Bei kila 12,000/ ya ng'ombe Tena utumbo (huyo mdada)anatulingishia?na mnajipa majibu wenyewe hata mimi sikutaka ku comment,Yanga Ni Timu ya kiume, wanawake siyo priority
ReplyDeleteIla mna timu ya wanawake!
DeleteMna timu ya kiume inayopigwa 4G na ya kike inaitwa princes imepigwa hamsa ama kweli Utopolo hamjitambui
Delete