MWINYI Zahera, ametambulishwa rasmi ndani ya Klabu ya Gwambina FC ambayo imepanda daraja msimu huu wa 2019/20 na itashiriki Ligi Kuu Bara msimu wa 2010/21.
Habari zinaeleza kuwa aakwenda kuwa kiongozi katika benchi la ufundi la Gwambina FC.
Zahera aliwahi kuifundisha Yanga ndani ya ligi msimu wa 2018/19 na alianza nayo msimu wa 2019/20 kabla ya kufungashiwa virago kwa kile kilichoelezwa kuwa aliboronga kwenye michuano ya kimataifa.
Zahera amesaini dili la awali kabla ya kutimiza vigezo alivyopewa huku akitajwa kuanza na ishu ya usajili.
Wanaotajwa kuibukia Gwambina ni pamoja na Mrisho Ngasa na Kelvin Yondani ambao kwa sasa ni wachezaji huru.
Gwambina wameramba dume
ReplyDeleteHii gwambina inatoka mkoa gani!
ReplyDeleteTutegemee kila la heri kwa Gwambina kutokana na umakini wa Zahera
ReplyDeleteAnaenda kuharibu team huyo
ReplyDeleteHofu yangu ni mmiliki wa hii timu akipata matokeo tofauti ya kamati kuu kupitisha majina ya wagombea Ubunge, Gwambina isijetelekezwa kama Singida United.
ReplyDeleteAcheni ujinga gwambina inauwanja wake mzuri tu kuliko hata Yanga acheni husda.itabirie gwambina kufanya makubwa kuliko hata Namungo.
ReplyDelete