LEO Agosti 7, uongozi wa Klabu ya Yanga umetangaza rasmi kuachana na nyota wao wawili, Kelvin Yondani na Juma Abdul baada ya kushindwa kufikiana makubaliano.
Wakongwe hao ndani ya Yanga mikataba yao ilikuwa imefika ukingoni msimu wa 2019/20 na taarifa ya awali ilielezwa kuwa walikuwa kwenye mazungumzo ya kuongezewa mkataba ila hali imekuwa ngumu kwa pande zote kushindwa kuelewana.
Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji hao walikuwa tayari kusaini dili jipya na walikuwa wakihitaji kupewa ada ya usajili huku Yanga ikielezwa kuwa walikuwa wanahitaji kuwapa mshahara na mkataba bila fedha za ada ya usajili.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, Abdul alitoa jumla ya pasi sita za mabao kati ya 45 yaliyofungwa huku akiaanza kikosi cha kwanza kwenye mechi 28 na Yondani alianza kikosi cha kwanza mechi 22.
Jumla Yanga inakuwa imeachana rasmi na nyota wake 9 ambao mikataba yake imeisha ndani ya Yanga.
Wakauze mchicha
ReplyDelete