August 30, 2020

 


MJUMBE wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia mshambuliaji wao kipenzi raia wa Burkina Faso, Yacouba Sogne atatua nchini Agosti 31, mwaka huu.

 

Agosti 27 mashabiki wa timu hiyo walijitokeza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINA) jijini Dar kumpokea mshambuliaji huyo ambaye baadaye ilishindikana kuwasili.

 

Yacouba ni kati ya washambuliaji wa timu hiyo waliosajiliwa akitokea Asante Kotoko ya Ghana mara baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na timu hiyo, kama mchezaji huru.

 

Kwa mujibu wa Hersi, ndege yake ilizuliwa kutua nchini hivyo amekatiwa tiketi nyingine na atatoka kwao Burkina Faso Agosti 31, mwaka huu kabla ya siku inayofuatia kutua nchini.

 

Hersi alisema kuwa mshambuliaji huyo mara baada ya kutua nchini, haraka ataungana na kambi ya pamoja kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

 

“ Hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya mashabiki na uongozi, kwani ndege aliyotakiwa kuja nayo Yacouba ilizuiliwa kutua nchini kutokana na sababu zao.

 

“Hivyo atajiunga na timu Agosti 31 na hatakuwepo kwenye kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa” alisema Hersi.

 


2 COMMENTS:

  1. Ww mwandishi mbona huelewek? Juz umetuambia kua anakuja tar 30 leo leo tena unatuambia tar 31 maana yake nn? Acha ujinga wa kutoa taarifa ambazo huna uwakika nazo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aliyesema ni msemaji wa Yanga na wala siyo mwandishi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic