August 13, 2020

 

UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuanzia kesho Ijumaa, Agosti 14 utaanza kutambulisha wachezaji wapya ambao umemalizana nao kwa ajili ya msimu wa 2020/21 pamoja na kutambulisha uzi mpya watakaoutumia.

Miongoni mwa wachezaji wapya ambao wanatarajiwa kutambulishwa na Simba ni pamoja na Ibrahim Ame kutoka Coastal Union, David Kameta,'Duchu' kutoka Lipuli, Charlse Ilanfya kutoka KMC ambao wataungana na Bernard Morrison kutoka Yanga.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, leo Agosti 13 kwenye Ukumbi wa Hotel ya Serena, Manara amesema kuwa;"Kesho Ijumaa tutazindua nembo mpya ya klabu. Tumeiboresha ili iendane na soko la sasa. Baada ya uzinduzi wa logo mpya tutazindua jezi mpya ya Simba ya msimu na tunaanza kutanganza wachezaji wapya.

Pia Manara amesema kuwa Simba inaunga mkono jitihada za Serikali katika masuala yote ikiwa ni pamoja na masuala ya utalii hivyo amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya utalii.

"Katika kuunga mkono Serikali, Jumatatu na Jumanne kupitia matawi yote nchi nzima. Wanasimba wote tutembelee vivutio vya utalii. Ni siku maalumu Wanasimba kuunga mkono utalii wa ndani." amesema.



13 COMMENTS:

  1. bora afanya kazi ya utalii huenda akafanikiwa

    ReplyDelete
  2. Replies
    1. hajafanikiwa hata katika perfume alizomuibia yule jamaa wa Oman

      Delete
  3. Upuuzi tu hapo hamna kitu kutoka kwa zeruzeru huyo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sindano inaingia polepole usijitingishe itakuumiza

      Delete
    2. This comment has been removed by the author.

      Delete
  4. alipoita press conference tulifikiria kuna jambo la muhimu kumbe anatafuta kiki kwa serikali - manara ipo wizara kamili inashughulikia suala la utalii usiwafundishe kazi

    ReplyDelete
  5. Kweli nimeamini washabiki wa Yanga wamepaniki/hawawezi utani yani simba pamoja na utani wao wote lakini hawajawahi kumdaharau mshabiki au kiongozi wa yanga kwa ulemavu wake lakini hawa jamaa wa utopolo wengi. Kweli masokwe yapo mengi

    ReplyDelete
    Replies
    1. wee shemeji wa mzee Tozi, kumuita mwenzio sokwe ndio utani, kwani ilo analolisema ni uongo si ndio alivyoumbwa unataka tufiche alivyoumbwa si ukosefu kwa aliyetuumba

      Delete
  6. Ata kama wamenunua timu waalipe fedha zetu kwanza sisi tununue timu nyingine. Kubadili nembo ni mchakato sio kitu cha mtu mmoja. Timu hamjakamilisha kuilipia mnmeiteka mbele ya macho yetu. Tupeni pesa sisi tuanze Simba yetu. Mkitaka ata jina badilini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jina hawawezi kubadili ndio wanalopigia hela kupitia mikia. Watabadili majina yote lakn sio jina rangi. Hivyo ndivyo chambo kwa mikia

      Delete
  7. Utopolo inawahusu nini?Mba matatizo chungu nzima bado mnajaribu kurekebisha wengine. Hakuna timu inasajili wachezaji 22 mdimu mmoja. Timu inawaacha manahodha wote wawili halafu inategemea mafanikio. Upuuzi mtupu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic