August 29, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa utawakera wapinzani wao wote ndani ya msimu wa 2020/21 kwa kuwa ina kikosi imara na chenye wachezaji bora katika kila sekta.

 

Simba imesajili nyota wapya saba ambao iliwatambulisha Agosti 22, Uwanja wa Mkapa kwenye kilele cha Simba Day ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison, Charles Ilanfya, Chris Mugalu, Larry Bwalya, Joash Onyango, Ibrahim Ame na David Kameta.


Akizungumza na Championi Jumamosi,Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa watawakera wapinzani wao bila kuchoka ikiwa ni pamoja na watani zao Yanga kwa kuwa wana kikosi kipana ambacho kinawapa nguvu ya kutamba ndani ya uwanja.

 

“Nakwambia tutawakera watu ndani ya uwanja kwa kuwa benchi la ufundi litakuwa na kazi ya kuchagua wanataka kianze kikosi kipi cha Larry Bwalya ambacho ndani yupo Bernard Morrison ama cha Chris Mugalu na ndani yumo Clatous Chama.


"Kwa namna ambavyo wachezaji wetu walivyo hasa falsafa ya Simba kucheza mpira mwingi wa pasi, acha tu msimu uanze tutashuhudia mengi kweli, hao wenzetu tutakutana nao tu,” alisema Manara.

14 COMMENTS:

  1. Safi kabisa safari hii mtu kafungwa chache kabisa ni 4G

    ReplyDelete
  2. Kipimo Vitalo siyo?Bt tunaomba msaada wa refa usiwepo pamoja na uswahiba

    ReplyDelete
  3. Kweli ndugu blog toka asubuhi matokeo ya ngumi za Jana bado issue nini lkn Simba sijui Bwalya mpaka unarudia rudia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu mwandishi lofa na uchwara sana! Kama ana elimu hata ya sekondari basi vyeti ni vya forgery! Nilimshangaa akimhoji mchezaji: "Did you add a new contract?" Eti mwandishi aliyekwenda mpaka mashindano ya fainali za CAF. MY FOOT. Anaaibisha sana Tanzania!

      Delete
  4. KUNA KLABU Hapa NCHINI MSEMAJE WAKE ANAFANANA NA NGURUWE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kosa kubwa sana kumfananisha mwanadamu mwenzako na mnyama/nguruwe. Tusiwe na ushabiki mpaka wa kujiondoa na na kuwaondoa wenzetu kwenye ubinafamu. Ni dhambi kubwa sana na kama Muislam unatakiwa utubie kwa Mola wako na kulia kabisa maana umefanya kosa kubwa sana. Hata kibinadamu tu mbali na dini umefanya makosa

      Delete
    2. Well said, hii tabia ya kutukana matusi sio Nzuri, na haifai kabisa.

      Delete
    3. Kwanza unaandika kwa herufi kubwa.Inakera kuandika kwa herufi kubwa...Herufi kubwa inamaanisha kupaza sauti, kufoka au kupayuka.inawezekana kabisa huyu ni mmoja ya wale mashabiki wa Yanga ambao Eymael aliwaita majina akisema kuwa ni mbumbumbu na.......sihitaji kurudia

      Delete
    4. Nikusahihishe kidogo hapo ndugu yangu, hilo jina la mbumbumbu alilitumia Aden Rage kuwa-"characterize" wanachama wa Simba! Inaonekana umelewa gongo wewe!!

      Delete
  5. wakereni kabisa kwani wanakera sana.
    eti kocha wao alibeba klub bingwa afrika akiwa na TP Mazembe!Sasa Sven alibeba alibeba Africa cup of Nations! Eti Sven alipotoka aliachishwa baada ta kushindwa kazi
    Chipolopolo ya kuifikisha Zambia finals! Sasa Mbona huko huyo kocha wa Yanga alikotoka ameacha timu ikiwa vobonde wa ligi kama Singida United...Timu ya mwisho kabisa katika ligi...wanatafuta ya Singida United ....watayapata tu.
    Eti wanataka milioni mia sita za Morrison. hata shilingi mia sita hawatapata! Wanakera sana hao

    ReplyDelete
  6. Wanaofanana na wanyama wa aina hiyo ni wale aliowasema aliekuwa kocha wao,wasiwapakazie wengine uhalisia wao

    ReplyDelete
  7. Kumwita nguruwe siyo kosa kwasababu tabia zake na akili zake zinajaa na kupwa na nguruwe vile vile,humu usituletee mambo ya dini .Kama ni tusi mbona mnajiitA Simba angeitwa Simba ungefurahi
    Mikia Fc

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi ni mwanayanga na sijaongea hayo kama nipo Simba. Wewe ukifananishwa na nguruwe utafurah? Tuache mambo ya ajabu kisa ushabiki. Mimi ni Mwanajangwani na sijawah kuifurahia simba kwa namna yoyote hata kwa bahat mbaya ila sijapenda kumfananisha mwanadamu mwenzangu na nguruwe. Huyobunayemzungumzia kweli anamadhaif kitabia na kimatamshi ila isiwe sababu ya kumwita nguruwe kwa sababu hata ww unatabia zako na lugha zako zisizofaa kwenye jamii na ndio maana ukadiliki kumfananisha mwanadam mwenzako na nguruwe

      Delete
  8. Best Hiyo ya Kingereza kwa Watanzania wote Ni issue,tunajua Sana Eng/Swahili ,labda Watoto wetu , Samahani yupe jamaa wa Azam TV Ndo alitoa Kali siku ana mhoji Kocha wa Simba Sumbawanga. Hiyo lugha na nguo alizovaa tofauti na fani yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic