August 17, 2020

 

Uzi mpya rangi nyeupe wa Azam FC ambao utatumika msimu wa 2020/21 kwa mechi za nyumbani pia upo wa bluu ambao utatumika kwenye mechi za ugenini na Azam FC wa ziada kwao ni rangi ya chungwa.


Jana, Agosti 16 uzi wa Azam FC ulizinduliwa rasmi pale makao makuu ya Azam FC,  Chamazi na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wilfred Kidao.


Ilikuwa ni kwenye tamasha la Azam Festival ambalo ni rasmi kwa ajili ya kutambulisha wachezaji na kilele chake kinatarajiwa kuwa Agosti 23.


Siku ya kilele Azam FC watatambulisha uzi wao tena na watacheza mechi na timu ya kimataifa ikiwa ni kwa ajili ya kufungua rasmi msimu wa 2020/21 na kutambulisha wachezaji wao wapya na wale wa zamani.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic