August 19, 2020

 


NYOTA wapya ambao wamemalizana na Yanga hivi karibuni, nchini Congo, leo Agosti 19 wameanza safari kutoka nchini Congo, kuitafuta ardhi ya Tanzania ili kujiunga na wachezaji wenzao ambao wameanza mazoezi.

Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko wote nyota wa zamani wa AS Vita wamemalizana na Yanga kwa kusaini kadarasi ya miaka miwili wanatarajiwa kuibuka ndani ya ardhi ya Tanzania, kesho Agosti 20.

Leo wanatarajiwa kupumzika nchini Ethiopia kabla ya kuanza safari kesho kwa ajili ya kuja nchini Tanzania.

Wachezaji hao wawili wapo bega kwa bega na Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said ambao ni wadhamini wa Yanga na ndio ambao wamefanikisha suala zima la usajili wa wachezaji hao.

 .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic