Kahata aliibukia nchini Kenya baada ya Simba kutwaa taji la Kombe la Shirikisho kwa kuifunga Namungo FC mabao 2-1 ambapo wachezaji walipewa mapumziko ya wiki mbili.
Kwa sasa Simba imeanza maandalizi ya ligi pamoja na kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Vital'O ya Burundi utakaopigwa Agosti 22, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni kilele cha Simba day.
Pia Simba itautumia Uwanja wa Uhuru ambapo watafunga 'Big Screen' kwa ajili ya mashabiki kuona shughuli zinazoendelea Uwanja wa Mkapa na kiingilio chao Uwanja wa Uhuru itakuwa ni buku mbili tu.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wamejipanga kutoa burudani.
0 COMMENTS:
Post a Comment