August 17, 2020

  


TAARIFA za uhakika zinaeleza kuwa Yanga imemaliza na AS Vita na kumsajili mshambuliaji kinda wa AS Vita ya DRC, Tuisila Kisinda.


Shughuli hiyo imefanyika jijini Kinshasa, DRC na Yanga imewakilishwa na Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa uwekezaji wa Kampuni ya GSM.

Mtu wa karibu na Kocha Mkuu wa AS Vita amesema kuwa sababu kubwa iliyompeleka kigogo huyo wa GSM ni kumalizana na wachezaji anaowahitaji kwa ajili ya kuimarisha nguvu ndani ya kikosi cha Yanga.

"Amekuja kiongozi kutoka Yanga ambaye ni mkubwa na ameongea na Kocha Mkuu wa AS Vita ili kupata wachezaji wawili kutoka Congo, hivyo ninaamini kwa kuwa wamekuwa na ukaribu kwa muda na wamezungumza mengi ni suala la kusubiri tu," ilieleza taarifa hiyo.

9 COMMENTS:

  1. hv ninyi ni waandishi ai ni makanjanja? unandika ujinga gan huu?

    ReplyDelete
  2. Kwamba kiongozi ameongea na kocha Wa As vita kuhusu upatikaji Wa wachezaji, duu hiyo hatari !!!sasa wewe unajuaje kama ni Kissinda

    ReplyDelete
  3. Anampigia debe Simba,maana yeyote anayesemekana kumalizana na Yanga Simba hawamwachi

    ReplyDelete
  4. Hahahaha aiseee huyu mwandishi ni mavi kabisa ingawa jamaa amesajiriwa tayari lakini hiyo nukuu ni ya ujinga sana

    ReplyDelete
  5. Kwa io kufanya usajili unaongea na kocha. Duh hatareeee

    ReplyDelete
  6. Ndio waandishi wa kiBongo, habari zao nyingi za kuungaunga tu, habari hazitoshi kuwa reference Mpaka uangalie sehemu nyingine

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic