August 17, 2020

 


KIKOSI cha Simba leo Agosti 17 kimeanza maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara pamoja na mechi yao ya siku ya Simba day inayotarajiwa kuchezwa Agosti 23, Uwanja wa Mkapa.


Wachezaji wa Simba wameripoti kambini leo na kuunganisha moja kwa moja mazoezini kwenye uwanja wao uliopo maeneo ya Bunju.


Bernard Morrison kiungo mpya wa Simba ambaye ametokea Klabu ya Yanga alikuwa akionekana ni mwenye furaha huku akicheza  wakati walipokuwa wakienda kambini.


Ameungana na wachezaji wenzake wapya ambao wamesajiliwa kwenye dirisha kubwa lililofunguliwa Agosti Mosi na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.

Wachezaji hao ni pamoja na Larry Bwalya, Joash Onyango,Chris Mugalu, Charlse Ilanfya, Ibrahim Ame na David Kameta.

3 COMMENTS:

  1. Yanga walikuwa wanamtaka Deo Kanda wa Simba kwa udi na ubani lakini Hawa kumpata. Habari zinasema kuwa Simba wameamywa kumrejesha Kanda Mazembe kwasababu Mazembe nao walidii nao wapewe dau kama lile alilopewa Dau ili wamuache kwahivo Simba ikaamuwa kuwarudishia Mazembe na kuleta mchezaji mwengine bora na mdogo kwa umri kuliko Kanda, kwahivo sasa njia nyeupe kwa Yanga wamchukue wao kilaini

    ReplyDelete
  2. Hahhh yanga tunaleta kitu machinery

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic