UONGOZI wa Klabu ya Yanga umewaomba mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Agosti 30, Uwanja wa Mkapa kwenye kikele cha wiki ya Mwanachi.
Siku hiyo Yanga imepanga kuwatambulisha wachezaji wapya na wale ambao walikuwa ndani ya kikosi kwa msimu wa 2019/20 watakaoendeleza gurudumu msimu mpya 2020/21.
Pia kutakuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya kimataifa kutoka Burundi huku burudani zikitolewa na wasanii ikiwa ni pamoja na Shilole, Madee, Chege Chigunda na Harmonize.
Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa:"Tunawaomba mashabiki na wadau wa Yanga wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa kwani kuna jambo letu muhimu.
"Malengo makubwa ni kuona kila mmoja anafurahi kuona timu yake ikiwa uwanjani na kuwaona wachezaji bora kwani usajili wetu ni makini na kila kitu kipo sawa."
Miongoni mwa nyota ambao wamesajiliwa na Yanga ni pamoja na Fernandes raia wa Angola, Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko raia wa Congo, ambao ni nyota wa kigeni huku wazawa ni Farid Mussa, Abdallah Shaibu, Bakari Mwamnyeto na Waziri Junior.








Magazet yaliwasajilia Yacob,Kotei,Makambo,Ali Nionzima(Azam)kweli team ya vyombo vya habari maneno mengi.
ReplyDeleteHivi uko na kichwa timamu? Umesema magazeti co club iliwasajiri saa nyingine unazi tujaribu kuweka kando tuongee ukweli.
ReplyDeleteKichwa timamu kipi unachotaka kwani hayo ya kina Kotei ya uongo?
ReplyDeleteKichwa chako kweli ulisha vita ,maana unaishi kwa steam ,watu wanaongelea hili wewe sijui Makambo sijui gazeti, Sasa wewe wapi Walter Bwalya au Shonga cse Magazeti yaliandika
ReplyDeleteKwahiyo Hiyo akili ya Kama mpiga chabo umeona Yanga kutosajili hao imekwama,au kwasababu walioletwa huwajui mpaka ustue.
ReplyDelete