September 23, 2020


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema kuwa kwa msimu wa 2020/21 ikiwa itatokea timu itaingia kichwakichwa kucheza na Klabu ya Simba itaokota mabao mengi nyavuni.

Biashara United mchezo wake wa kwanza nje ya Mara, ilikutana na Simba ambapo ilifungwa mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Septemba 20.

Kichapo hicho ni cha kwanza kwa Biashara United kupokea kwa msimu huu mpya kwa kuwa ilicheza mechi mbili bila kufungwa bao lolote na ngome ya Daniel Mgore kuwa imara kwa muda wa dakika 180.

Baraza alianza kumenyana na Gwambina FC Uwanja wa Karume kwa kushinda bao 1-0 kisha ikamaliza safari yake mbele ya Mwadui FC kwa kushinda bao 1-0 kabla ya kuondoka Mara kuifuata Simba.


Baraza amesema:"Simba ni timu kubwa ambayo inafanya vizuri katika mechi zake, lakini ikitokea timu ikaingia kichwakichwa inaweza kufungwa mabao zaidi ya yale ambayo sisi tulifungwa.


"wachezaji wangu walikwama katika kutegua makosa yao ambayo waliyatega wenyewe na nafasi ambazo walitengeneza walishindwa kutumia hilo linatufanya tuanze kujipanga upya kwa ajili ya mechi zetu zijazo.


"Bado kwa sasa ligi inaanza tuna nafasi ya kufanya vizuri hakuna haja ya kukata tamaa imani yangu ipo kwa wachezaji na nguvu ya kufanya vizuri ipo," amesema.


7 COMMENTS:

  1. Yanga ya tieni akilini anayokwambieni kocha wa Biashara na wala msiseme kama kawaida yenu kuwa Myama kanunuwa mechi au wamependelewa.

    ReplyDelete
  2. Watakubali taratibu Ukweli na uwazi utajulikana .Simba ni level nyingine lakini makanjanja hawakubali. Ile pasi ya Chama angetoa mchezaji wa timu fulani zingeandikwa makala chungu nzima na hawa makanjanja.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Walianza kusifia wachezaji kwa kupiga kona sasa hivi limewashuka baada ya Chama kuonyesha vitu vyake wanaanza kuleta story za uongo

      Delete
  3. Simba is the next level,; Simba ndo team yenye mashabiki wengi mitandaoni ikifuatiwa na national Al haly. Mpaka Afrika yote wanaishabikia Simba na kuifuatilia acha kabisa. Hawa viazi wengine wanaajiri wasemaji hamsini kdg lkn sifuri Hamna chochote!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic