MMOJA wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Zacharia Hans Poppe, kama ameimpa mechi 10 tu timu ya Yanga ambayo inatamba na kiungo mshambuliaji wao, Carlos Carlinhos.
Carlinhos ni kati ya wachezaji gumzo hapa nchini kwa sasa akiwa amefanikiwa kutoa pasi moja ya bao kwenye mchezo mmoja wa ligi aliocheza akiingia akitokea benchi.
Wikiendi iliyopita alikuwa gumzo baada ya kuisaidia timu yake ya Yanga kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Hans Poppe amesema ni mapema mno kuweza kuzungumzia viwango vya timu na wachezaji kwa sasa kwa kuwa hazikwenda katika maandalizi ya msimu mpya ‘Pre Season’.
Ligi ni ngumu kila timu inahitaji kuona inafanikiwa kufanya vyema huko mbele, lakini ni mapema mno kuweza kutoa tathimini ya mchezaji mmoja mmoja na timu kwani hakuna ambayo ilikwenda kufanya Pre Season kwa kuwa muda ulikuwa hautoshi.
“Hivyo ni mapema mno kuelewa itakuwaje na nani staa kwa sasa hadi mechi ya 10 huko ndio timu zitaanza kuwa na ushindani na itafahamika nani ni staa na timu gani ni bora, kwa sasa ndiyo maana timu nyingi hazifanyi vizuri,” alisema Hans Poppe.
Chanzo: Championi
Hans Pope ameongea kiufundi sana na weledi wa hali ya juu katika soka kiujumla japokuwa kama kawaida ya waandishi wa hii blog wamepachika kichwa cha habari ambacho hakihusiani na habari yenyewe maana hakuna sehemu alipoitaja Yanga kama timu pekee inayohitaji mechi kumi kukaa sawa lakini makanjanja wa Saleh Jembe wanakandika tu matope yao kwenye blog
ReplyDeleteTCRA waanze na hawa jamaa maana uandishi wao hauna weledi wala kiwango hata kidogo!!!!
ReplyDeleteHans pope hana maadili mrubuni Wachezaji ,kwanini awekwe yeye .Mpe namba ya huyo mchezaji ulo mtaja lkn sijui Kama atakubali kuwasaidia Kama ile mechi mlotufunga nne.
ReplyDelete