September 19, 2020


 OFISA Habari wa Simba SC, Haji Manara amesema Bodi ya Ligi (TPBL) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wameridhia maombi ya kushusha viingilio vya mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

Hata hivyo, baada ya Simba kusema hivyo gumzo kubwa limezuka kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya mashabiki wakiwakejeli kuwa wamepoteza mvuto.

 

Awali katika michezo ya Simba viingilio vilizoeleka kuwa ni 5000, lakini mpaka sasa timu hiyo imewasilisha maombi hayo ambayo huenda yatakuwa na tija kwa mashabiki wao.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Manara, alisema kuwa tayari klabu hiyo imewasilisha maombi hayo kwa TPLB pamoja na TFF kwa ajili ya kupunguza viingilio hivyo kwa ajili ya kuleta hamasa kwa mashabiki wao.

 

“Tuna furaha wenzetu wa Bodi ya Ligi na TFF kuridhia maombi yetu ya kutaka mechi hizi za Dar es Salaam ili kuongeza hamasa zaidi kushusha viingilio hususani vya mzunguko, awali tulikubaliana kimsingi na Bodi ya Ligi na TFF kiingilio cha chini kitakua 3000 kutoka 5000.

 

“Taarifa rasmi ya aina ya viingilio na majukwaa yake kwa mchezo unaokuja tutatangaza kwenye kurasa zetu za Instagram za klabu lakini kwa sasa kiingilio cha chini ambacho tulitaka kishushwe zaidi kinaweza kuwa 2000 hadi 3000 na tutaridhika nacho,” alisema Manara.

 

Kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa VPL, Simba kwa sasa kipo kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa raundi ya tatu dhidi ya Biashara United utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar saa 1:00 usiku na hapo ndiyo viingilio vipya vitatumika.


 Tayari kwa sasa imeshakuwa rasmi kuwa mechi ya kesho kati ya Simba na Biashara United itakuwa kiingilio cha mzunguko ni buku tatu jambo ambalo limekuwa gumzo kwenye mitandao kwa baadhi ya mashabiki wakiendeleza kejeli zao za kiutaniutani.

9 COMMENTS:

  1. Inamaana nyie hamjaelewa sasa hvi hawana mashabki wameamua kufanya hvyo iliwaonekane wanajaza uwanja wameishiwa mashabiki japo wana kikosi cha akina (kaopwa) sa hvi mashabki mnatkiwa kujua Timu ya simba ni KAOPWA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie kama mna mashabiki mbona mechi zenu mbili za ligi mmeshindwa kujaza uwanja aliyewaita manyani uneducated hakukosea

      Delete
    2. Yani Simba inakera hadi baadhi ya vyombo vya Habari vimeamua kuanzisha mkakati wa kushindana na simba kuleta mfarakano ili waisaide Yanga kupata ubingwa mmechelewa kweli, matokeo ya uwanjani ndio yanawavuta washabiki. Alafu ukitaka kujua hizi ishu zinapikwa na waandishi wa Habari ninavyojua mimi Tanzania hatuna utamaduni wa kujaza viwanja mechi za ligi sasa huo mvuto ianosemekana simba imeupoteza sijui imetokea wapi.

      Delete
  2. Utopolo tumewazoea.Baada ya muda visingizio vitaanza.

    ReplyDelete
  3. Simba haiendeshwi kwa gate collection ina vyanzo vya mapato lukuki hivyo kufurahisha mashabiki ni sera yetu. Uchumi mgumu lazima tuone jinsi ya kuwaenzi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mnachosema nikweli mnavyanzo vngi vya mapato kama juice,sabun nk watoto wa mo nilazma m2nzwe kama ilivo andkwa kwenye sheria ya mtoto kua ni wajbu wa mzazi kutunza familia yke ko nampongeza mo kwa kutimiza wajbu wake

      Delete
  4. Mbona sioni tatizo, mechi 8namhusu simba, hata wakitaka mashabiki waingie bure sawa tuu ili mradi simba walipie gharama za uendeshaji. Yanga kama wanaona wananchi wanauwezo waweke biingilio hata laki poa tuu

    ReplyDelete
  5. Noana sasa hivi Taarabu fc wameshindwa kucheza mpira uwanjani sasa wanataka kushindana na Simba kwa maneno (Taarabu), wao wanaosema timu yao ina mvuto kwa kipi matokeo ya uwanjani Simba bingwa mara 3 mfululizo, simba ndio wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Klabu bingwa Africa. Wao kama timu yao ina mvuto wa washabiki tutaiona baada ya mechi 8 tu, ndio tutajua timu ipi ina mvuto kwa washabiki, huo ushabiki wa mihemko kwa kusifiwa kwenye magazeti tutauona kama mtaendelea hivyo hivyo kuja uwanjani muda utaongea

    ReplyDelete
  6. kuna mbinu chafu zinazofaywa na baadhi ya vyombo vya habari kuididimiza simba hii ikiwa ni moja ya mikakati ya timu pinzani kushusha umoja wa timu wakilenga kuvuruga juhudi za kutetea ubingwa hii inafanyika kwamakusudi kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic