September 23, 2020


 MKURUGENZI wa Uwekezaji wa  GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa matokeo chanya ambayo wanayapata Yanga kwa sasa kwenye mechi zao tatu zilizopita yanawapa matumaini ya kuendelea kufanya vizuri.


Yanga ikiwa imecheza mechi tatu za ligi, imeshinda mechi mbili na kulazimisha sare moja ambapo kibindoni imefunga mabao matatu na kati ya hayo mawili yakifungwa na wachezaji wapya wawili ambao ni Tuisila Kisinda na Michael Sarpong.


Hersi amesema kuwa kwa namna ambavyo wachezaji wanapambana ndani ya uwanja kunawapa matumaini ya kufikia malengo yao waliyojiwekea.

“Ni faraja kubwa kuanza kupata matokeo baada ya kile ambacho tulitarajia kukifanya msimu huu. Timu yetu tuliijenga na tuliangalia kufanya makubwa kwenye kila idara ikiwa ni kuifanya timu irudi kwenye ubora.

 

“Tunachotaka ni kuendelea kupambana zaidi kwa ajili ya kufanikisha ndoto za kuwa mabingwa kwa msimu huu na bado tunaona kikosi hakijawa sawa kikiwa kamili zaidi kwa maana wakijuana basi tutakuwa na uwezo wa kufanya makubwa kuliko ilivyo kwa sasa,” alimaliza Hersi.


Mchezo wa Yanga unaofuata Septemba 27 kitamenyana na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

14 COMMENTS:

  1. Ukweli tukiweka ushabiki na unazi pembeni, tuongelee uhalisia na kama kocha mwenyewe wa Yanga aliwakunukuliwa akizungumzia uwepo wa bahati kwenye matokeo ya mpira wa miguu, basi ukweli Yanga imekuwa ikishinda kibahati bahati na timu bado haijakaa sawa kiufundi na kimbinu, mimi naona ipo haja ya kufanya maamuzi magumu katika benchi la ufundi ilhali bado ni mapema, kwani kauli ya kusema kocha bado anatafuta muunganiko itaendelea kuwapumbaza na viongozi wakijastuka kutaka kubadili benchi la ufundi, pengine Yanga itakuwa inapigana kutokushuka daraja au ikaishia nafasi ya 6,5 au 4. Tusijidanganye na matokeo haya tuliyoyapata sasa, timu haipo sawa, Yanga inashinda kwa uwezo binafsi wa Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Yasin Mustapha, Kibwana Shomary na Feisal Salum, hawa ndio wanaibeba Yanga na kufunika udhaifu mkubwa wa kocha mkuu na msaidizi wake, Yanga inatumia uwezo binafsi wa wachezaji kushinda, haichezi kitimu, haina muunganiko na haina mfumo unao eleweka kiuchezaji, kutafuta muunganiko sio kazi ya siku moja lakini sio kazi ya zaidi ya wiki mbili kama wachezaji uliowasajili kweli ni professional, ndio maana nasema Yacouba Sogne hana kiwango cha kuchezea timu inayotaka kuchukua ubingwa mbele ya Simba na Azam nadiriki kusema Waziri Junior ni bora sana kuliko Sogne, Sarpong anacheza na jukwaa hana msaada ni mbinafsi fulani mjivuni ni bora Waziri Mahadhi aanze kupewa nafasi ili ajenge hali ya kujiamini huyo Sarpong ni Molinga namba 2, Carmo si mchezaji wa kucheza mechi ngumu kama za Simba na Azam, yupo na kipaji na akili ya mpira ila ana nguvu ya kupambana ktk mechi ngumu ni bora kumtumia Farid Mussa kuliko huyu muangola. Najua comment yangu mtaipinga sana ila hifadhini comment hii, mwisho wa msimu mtairudia na kuamini nilichokisema hapa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe hujui mpira na nadhan hujawah hata kucheza mpira wa makaratasi. Kwenye mpira unatakiwa wachezaji wazoeane kimbinu na kiuchezaji na kocha anapaswa kuwajua wachezaji wake

      Delete
    2. kuna siku utaelewa najua mpira ama sijui na siku si nyingi majibu utayapata, jumapili utazame mpira wa Yanga na Mtibwa kwa umakini sana, weka ushabiki pembeni utazame mpira kama mwanamichezo hakika utajua kwanini nimeandika haya. Mimi ni Yanga na ninajua uelekeo tunao elekea sasa una maumivu makubwa ipo siku watu hawataonekana uwanjani Yanga ikicheza. Tuna haki ya kukosoa na kuongea kwa yale tunayo ona yana mapungufu. Time will tell, let us wait.

      Delete
    3. Nimekupata boss, hata mimi nilikuwa najiuliza hasa kigezo kilichotumika kumpata kocha msaidizi, kwani hata historia yake na timu aliyokuwanayo haiko njema, maboresho zaidi ni benchi la ufundi kabla ya kuangalia sehemu nyingine

      Delete
  2. Wewe mikia jidanganye kumfunga stend ndio unaona unatimu yanga ratiba yake ameanza na timu andamizi kwenye ligi chambua kisoka mpaka michi ya nne simba atakuwa kacheza na timu ngumu 1 tu mtibwa yanga zote 4 ngumu usisifu makali ya kisu kwa kukata mkate

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww umecheza na team majina, kagera mechi tatu anapoint gapi, mbeya city naye anapoint nagapi? Acha kuropoka kunazi angalia uhalisia na majira usika team IPO wapi kwakiwango majira hayo.

      Delete
  3. Hivi Mbeya city na Kagera msimu huu Ni timu ngumu?acha ushabiki mandazi mjibu muhusika kwa hoja

    ReplyDelete
  4. Yanga ina uongozi mzuri (good management) ambao umejipanga vizuri kiutendaji (well organized team work) Yanga ina baadhi ya wachezaji wazuri sana, wengi ni vijana wadogo wenye kuweza kufundishika na kushika mafunzo kwa urahisi, miili yao inakubali mazoezi kirahisi na wana kiu ya kupata mafanikio makubwa, wachezaji baadhi wako ok, kama asilimia 90% ukimtoa Yacouba Sogne. Ila Benchi la ufundi la Yanga ndio kansa itakayoitafuna Yanga msimu huu, ni benchi lisilokuwa na mbinu na zaidi litategemea vipaji vya wachezaji ili kulinda ajira zao, ni makocha wanaojificha nyuma ya wachezaji ili wapate mafanikio, watategemea zaidi jitihada za baadhi ya wachezaji ili kupata matokeo uwanjani, sio kwa mbinu na ufundi wao ambao umepitwa na wakati na hawana mbinu mbadala za kuwapa wachezaji. Bado ni mapema kuweza kufanya mabadiliko na ni vizuri zaidi ikiwa nia ni kushinda ubingwa wa vpl au fa cup, viongozi wakichelewa kubadilisha benchi la ufundi hakika watakuja jutia subira yao, mechi na mtibwa itakuwa ni kipimo tosha, kadri timu itakavyozidi kufanya vibaya, morali ya wachezaji itashuka, morali ya mashabiki itashuka, hata mwitikio wa mashabiki kununua jezi na kujaa uwanjani utapotea na GSM watapata hasara kubwa kiuchumi, kosa litakuwa limeanzia kwenye benchi la ufundi, benchi la ufundi ni kitengo muhimu sana kwenye timu, ufanisi wa timu uwanjani unategemea ubunifu weledi na ujanja wa kimbinu wa benchi la ufundi, ndio maana huko duniani katika timu kocha ndio wa kwanza kuwajibishwa na wakati mwingine kocha anafukuzwa kwakuwa timu haichezi soka la kuvutia bila kujali matokeo, kwasababu hao matajiri na wawekezaji wa hizo timu uangalia faida kibiashara, yaani timu ishinde icheze mpira mzuri mashabiki waongezeke (fan base) iwe kubwa na fan base ikiwa kubwa hiyo ni jukwaa la kibiashara kwa wao kujitangaza na kuitangaza timu na hapo uchumi wa klabu na mdhamini unaongezeka. Kocha ana athari kubwa kwenye mafanikio ya timu na wawekezaji kiujumla. Ndio maana matajiri wanao miliki vilabu hawanaga muda wa kumvumilia kocha anaefanya vibaya kwakuwa wanajua timu ikifanya vibaya hata brand zao kibiashara zitashuka pia.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ulitaka wawe na mbinu gani hilo benchi la ufundi kwa mfano ili uthibitishe kuwa iko vzr?

      Delete
  5. Nyie mnaojifanya kujua mpira na kukosoa uwezo wa kocha na benchi zima la ufundi na hata baadhi ya wachezaji,mlicheza au kufundisha wapi mpira! Acheni kuingilia majukumu ya watu, rudini huko mliko toka rudini kwa hao waliowatuma. Na nyie wanachama na mashabiki wa kweli wa Yanga wapuuzieni hawa wanao'post' kwa lengo la kuanzisha chuki na vurugu klabuni.

    ReplyDelete
  6. Replies
    1. kaanzishe timu yako kwanza, halafu uifundishe ndipo tulinganishe

      Delete
  7. Endeleeni kujipa moyo Wana Yanga ila baada ya mechi kama saba hivi hakika mtabadili mawazo yenu na mtajua tulio kuwa tuna kosoa sio wote ni Simba wengine ni Yanga na tunajua nini maana ya mpira zaidi yenu. Tuendelee kutafuta muunganiko wa timu wakati wenzetu wana tafuta ubingwa kwa kuongeza pointi na magoli ya kutosha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo la mpira wa Tz lina watu wengi wanazi na wasiyopenda kusikia mtu anakosoa hata kama anachoshauri ni kweli. Ukiikosowa Yanga utambiwa mikia na ukiikosoa Simba utaitwa utopolo. Si ajabu hatuna mafanikio kimataifa maana tunataka kusifiwa hata kama timu ni mbovu kiasi gani. Acha tuendelee kucheza mpira kwenye vyombo vya habari

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic