September 23, 2020

 


TUISILA Kisinda winga mpya ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa wanajukumu kubwa la kupambana kwa ajili ya timu hiyo ili kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


Kisinda ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo aliibukia kikosini akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo pamoja na nyota mwenzake Tonombe Mukoko. 


Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ni wa raundi ya nne dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Septemba 27,Uwanja wa Jamhuri Morogoro. 


Kisinda amesema:"Wachezaji tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili ya kutimiza majukumu yetu ndani ya Yanga pamoja na kuwapa furaha mashabiki.

"Ipo wazi kwamba kila mchezaji anatambua majukumu yake na ni wazi kuwa kwenye ligi ushindani upo kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi kama ambavyo sisi tunahitaji."

Yanga ikiwa imefunga mabao matatu kwenye mechi tatu za ligi amehusika kwenye bao moja ambapo alitoa pasi moja ya bao wakati Yanga ikishinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar, Kaitaba. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic