September 10, 2020


 KIUNGO mpya wa Simba, Larry Bwalya, raia wa Zambia, amefunguka kuwa atapambana kuhakikisha kikosi hicho kinakuwa na mataji mengi kwa msimu huu.

 

Kiungo huyo ameongeza kwamba ana shauku kubwa ya kuwa sehemu ya mafanikio ya kikosi hicho kwa kuwa ni moja ya timu kubwa Afrika kwa kipindi hiki.

 

Bwalya aliyetua Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Lusaka Dynamos, tayari ameshatwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii na timu hiyo walioutwaa kwa kuifunga Namungo FC mabao 2-0 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Agosti 30.


Kiungo huyo Mzambia amesema kuwa kwake atapambana vilivyo kuhakikisha anakuwa moja ya sehemu ya kikosi hicho ambacho kitatwaa mataji mengi kwa msimu huu.

 

“Tangu nitue hapa Simba najisikia niko nyumbani na nitapambana zaidi kuona timu inafanya vizuri.

 

“Nina shauku ya kuwa sehemu ya moja ya timu ambayo ilifanya vizuri na kuwa na mafanikio kwa kutwaa mataji kwenye klabu hii ambayo ni moja ya timu kubwa kwa sasa Afrika,” alimaliza Mzambia huyo.


Kwa sasa Simba inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Septemba 12, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic