September 25, 2020


 

UONGOZI wa KMC umesema kuwa hauwezi kutaja sababu iliyowafanya wachezaji wake wakapita kwenye nyavu jana wakati wa kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.

Jana, Septemba 24 Klabu ya KMC wakati ikifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar utakaochezwa leo Septemba 25 wachezaji walionekana wakipita kwenye nyavu za uzio baadala ya kutumia mlango wa kuingilia uwanjani.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kwa sasa hawawezi kuzungumzia suala hilo mpaka watakapomaliza mchezo wa leo.


"Kwa wakati huu hatuwezi kuzungumzia suala la wachezaji kupita kwenye nyavu na badala yake tunajikita kwenye mchezo wa leo kusaka pointi tatu.


"Baada ya kumaliza mchezo hapo tutaweza kuzungumzia suala hilo," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic