September 25, 2020


MSHAMBULIAJI wa timu ya soka nchini Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya Uturuki Fenerbahce kwa mkataba wa miaka minne.

Samatta alikuwa anakipiga ndani ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England, ila kwa msimu wa 2020/21 alikwama kupenya kikosi cha kwanza kutokana na kushindwa kuonyesha makeke aliyokuwa nayo awali.


Aliibukia ndani ya Aston Villa akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na ni mtazania wa kwanza kucheza Ligi Kuu England ambayo ni namba moja kwa kufuatiliwa duniani.


Akiwa ndani ya Villa, Samatta aliweza kutupia mabao mawili na timu yake ilikuwa kwenye hatihati ya kushuka daraja ila iliponea kwenye tundu la sindano baada ya kushinda mchezo wake wa mwisho.

Akiwa Villa alicheza jumla ya mechi 16 na alitupia mabao mawili kwa nafasi yake.

Samatta amesema kuwa anafurahi kupata changamoto mpya na anaamini kwamba utakuwa wakati wake bora wa kufanya vema ndani ya timu yake mpya.

5 COMMENTS:

  1. Inauma sana Samatta kutoendelea kucheza EPL, ingawaje alikua katika kipindi kigumu sana, pressure ilikua ndani mpaka nje ya uwanja.
    Anyway maisha popote huenda safari hii ata shine Uturuki na kurudi England.
    Mwenyewezi Mungu amfanyie wepesi Mtanzania Mwenzetu.

    ReplyDelete
  2. Kaza buti kaza buti, huko utashine na epl utarudi kwa uweza wa MUNGU. Nakuomba ukafanye makubwa urudi kwakugombaniwa.

    ReplyDelete
  3. Nakuombea ukafanye makubwa urudi epl kwakugombaniwa na vigogo mbalimbali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic