September 3, 2020

 


MANCHESTER United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer imesimamisha mazungumzo ya kumpata kiungo wa Aston Villa, Jack Grealish na kumgeukia Donny van de Beek anayekipiga Ajax.


Awali ilielezwa kuwa United walikuwa wanataka saini ya nahodha huyo wa Aston Villa anakokipiga mzawa Mbwana Samatta lakini Solskjaer amesema kuwa anataka kumtazama yule wa Ajax.


United ilikuwa tayari kuweka mezani kitita cha pauni milioni 80 kupata saini yake. Kiungo huyo aliweza kuonyesha kiwango kikubwa msimu uliopita na alikiongoza kikosi chake kujinusuru kushuka daraja.


Pia mabosi wa United walikuwa wanahitaji saini ya Jadon Sancho wa Borussia Dortmund huko dili lilikuwa gumu kwa sababu ya dau walilotajiwa kuwa kubwa.

4 COMMENTS:

  1. Manchester United team yangu lakini wamezedi ubahili yaani makombe tutayasikia redioni sisi tutakuwa washiriki tu

    ReplyDelete
  2. Manchester United team yangu lakini wamezedi ubahili yaani makombe tutayasikia redioni sisi tutakuwa washiriki tu

    ReplyDelete
  3. Manchester United team yangu lakini wamezedi ubahili yaani makombe tutayasikia redioni sisi tutakuwa washiriki tu

    ReplyDelete
  4. Timu inaboa sana,tatizo wamiliki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic