September 3, 2020


 YACOUBE Sogne, nyota mpya wa Yanga ambaye alitua nchini Tanzania Agosti 31 akitokea Burkina Faso na kupokelewa na viongozi wa Yanga takwimu zake zinaonyesha kuwa ni mtu kwelikweli.

 

Yanga wamemsajili mchezaji huyo akiwa ni wa mwisho kabisa kwenye usajili huu mkubwa, ukiwa ni muda mfupi kabla dirisha halijafungwa.

 


Akiwa ndani ya Asante Kotoko ya Ghana, Sogne alicheza jumla ya mechi 26, ambazo ni sawa na dakika 2,340 alipachika mabao sita, na kutoa jumla ya pasi tatu za mabao akiwa na wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 260.


Mshambuliaji huyo mwenye rasta kichwani aliwasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na mamia ya mashabiki ambao walijitokeza na timu ya Championi pia iliweka kambi hapo ambapo aliongea kwa kusema:“Ninawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kunipokea na ninaahidi kufanya kazi kweli,”.

 

Tayari nyota huyo amekabidhiwa jezi namba 10 ambayo ilikuwa inavaliwa na nyota wa zamani wa timu hiyo, Tariq Seif ambaye mkataba wake uliisha na Yanga haikuwa na mpango naye.

6 COMMENTS:

  1. Hii n hatari kwel kwel,Bora hata molinga

    ReplyDelete
  2. Dah kweli nechi 26 goli chache hivyo afadhali papaa

    ReplyDelete
  3. Rekodi yke imeishia hapo au ndio timu pekee aliyochezea

    ReplyDelete
  4. Hivi huyu Jembe mbona anajitia ubwege unampa mtu sifa zahovyo kabisa ili utopolo wakupende duu unatisha usijaribu wala usijaribu kutoa sifa za hovyo kwa mchezaji yoyote wa mabingwa wa nchi kama kazi yake ni nzuri sema kweli kama ni mbaya sema ukweli.Molinga alicheza mechi ngapi na alifunga magoli mangapi chini ya shinikizo gumu la mashabiki watopolo,leo unatuambia mtu kacheza nechi 26 goli sita duuu unamwagia sifa hivyo threres something wrong in your mind.Sisi washabiki wa kweli tunachukia kufanywa kama watoto wadogo acha hizo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic