UONGOZI wa Simba umewataka mashabiki wake pamoja na wadau wa mpira kuacha tabia za ugomvi pamoja na kuhitaji kulipa kisasi kwa kugombana ndani na nje ya uwanja kwa kuwa sio asili ya mpira.
Jana baadhi ya mashabiki ambao walionekana kuwa ni wa Yanga Uwanja wa Jamhuri walionekana wakiwapiga mashabiki wa Simba kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mchezo huo Mtibwa Sugar ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Yanga. Leo Yanga imetoa taarifa kuhusu suala la mashabiki wake kufanya vurugu na kuwataka waache suala hilo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Klabu ya
Simba inaamini kuwa Bodi ya Ligi Tanzania itachukua hatua stahiki kwa timu
ambazo zinakiuka utaratibu.
Manara amesema:"Mashabiki wasifanye vurugu kwani athari yake
ni kubwa na kuna baadhi ya nchi mashabiki waliwahi kuzuiwa kwenda uwanjani.
Nawaomba mashabiki wetu na mashabiki kiujumla waache kulipa visasi.
"Mpira sio uadui mpira ni kiunganishi kwa watanzania bila kujali wapi unatoka na dini gani hivyo kikubwa ambacho kinatakiwa ni kuendelea kuwa mashabiki wa amani bila kupigana kwani hiyo sio asili ya mpira."
Hii fujo inafanyika mara ya ngapi au bodi ya ligi na tff hawajui sanasana watawapiga faini ambazo hazitaenda kwa waathirika ngoja na sisi tuwafundishe adabu kidogo
ReplyDeleteHakuna sababu ya kulipiza kisasi kwa watu washamba kama hao. Mpira sio ugomvi. Mpira ni furaha na sio karaha
DeleteMashabiki wa Yanga waangalie mechi kati ya Simba na Biashara. Wataona ni kwa namna gani mashabiki wa timu hizi mbili, Simba na Yanga, walivyokuwa wamekaa jukwaani pamoja hata goli lilipokuwa linaingia shabiki wa Simba alirukaruka kwa furaha hadi kugongeana mikono na wa Yanga kuonesha kuwa walikuwa wanafurahia mpira na si ushabiki wa "kishamba" wa kupigana.
DeleteHawa na wao inabidi wafundishwe adamu sio mara 1 ama 2 ni kila wakati wanatupiga inatakiwa na wao watandikwe sasa
ReplyDeleteKuna watu wanajiona ni wajanja lakini kwa hali halisi ni washamba.Tatizo kizazi cha sasa hawajui utani wa Simba na Yanga ulivyo,mbona sisi mashabiki wa zamani hatukuwa na hulka hizi za kishenzi!!Nikiwa ni mshabiki mhenga wa Yanga nimekuwa nachukizwa na vitendo hivi vya kipumbavu na nina hakika hata mashabiki wahenga wenzangu wa Yanga hawafurahii ushenzi huu.Naulaumu pia uongozi wa juu wa timu yetu kwa kutoa matamko mepesi ya kulaani vitendo hivi bila ya kuonesha ni kwa jinsi gani watahakikisha wanatoa ushirikiano wa kuwatia mbaroni wahusika pindi watakapoonekana wanafanya vurugu.Suala hili limeachwa kwa muda mrefu matokeo yake sasa limeanza kuota sugu.Yanga ilikuwa ina sifa ya kuwa na mashabiki wastaarabu na waungwana lakini sasa kumejitokeza kikundi cha wahuni wanaotaka waonekane ni wababe wa Yanga ilhali ni washamba wa ushabiki
ReplyDeleteUmesema kitu cha maana mashabiki wa simba simba na yanga ni watu wanaoishi pamoja inakuwaje tuanze kufanyiana fujo
DeleteMikia fc lazima mpigwe tu hadi muache kuinhilia mambo yasiyowahusu
ReplyDeleteWacha upumbafu wewe hujui mpira na kengo la kuanzidhwa mshindano ya mpira.
DeleteHao mashabiki wa yanga ni wapumbavu sana,kwani mpira cyo vita
ReplyDeleteHao mashabiki wa yanga ni wapumbavu sana,kwani mpira cyo vita
ReplyDeleteMashabiki WA simba Ni waungwana na uungwana Ni vitendo.
ReplyDelete