September 5, 2021


 BABA mzazi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta amefichua kuwa moja ya sababu inayopelekea kijana wake kushindwa kudumu kwenye timu alizojiunga nazo kwenye kipindi cha karibuni ni suala la umri wake kusogea na kupelekea kasi yake kupungua.


Samatta ambaye alizaliwa 
mwaka 1992, kwa sasa amefikisha umri wa miaka 29 alianza kucheza soka katika klabu ya African Lyon mwaka 2008 kabla ya mwaka 2010 kujiunga na Simba kisha kuelekea TP Mazembe mwaka 2011, ambapo alicheza hadi mwaka 2016, alipojiunga na KRC Genk ambayo mwaka jana ilimuuza kwenda Aston Villa ya Uingereza lakini hakuweza kudumu nayo kwani alitolewa kwa mkopo kwenda Fenerbache ya Uturuki ambayo pia imemtoa kwa mkopo kwenda Royal Antwerp ya Ubelgiji.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mzee Samatta alisema kuwa suala kubwa ambalo limepelekea mtoto wake kushindwa kudumu kwenye timu moja katika kipindi cha hivi karibuni limechangiwa na umri wake kuwa mkubwa licha ya kuwa bado anapokea ofa ya timu mbalimbali.

 

“Kikubwa ambacho kimepelekea Samatta kushindwa kudumu katika timu nadhani ni umri wake kwa sababu sasa hivi amefikisha miaka 29, hivyo kasi yake haiwezi kuwa kama ilivyokuwa zamani ingawa bado alikuwa akipokea ofa za timu nyingine kubwa kama Montpelier ya Ufaransa ilikuwa tayari kulipa pesa lakini wakala wake ameamua kumpeleka Antwerp kwa kuwa anatokea Ubelgiji na ile timu inashiriki Europa League.

 

“Siyo kwamba Fenerbache hakuwa anacheza siyo kweli kwa sababu alikuwa akicheza kutokana na wingi wa wachezaji ilikuwa lazima na wengine wacheze, angalia Aston Villa siyo kwamba alishindwa kucheza ila Watanzania walichangia kumuondoa pale kwa maneno yao waliyokuwa wakimtupia yule Jack Grealish ila sasa umri wake unachangia japokuwa uwezo wake wa kufunga bado upo,” alisema mzee Samatta.

10 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic