September 13, 2020


 
AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Yanga Uwanja wa Mkapa ni wa kimbinu zaidi na mpango wake wa kwanza ni kuona anaweza kufanikiwa mapema kuishinda.


Mbeya City ilianza kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 mbele ya KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Septemba 7.

Leo majira ya saa 1:00 usiku ina kibarua cha kumenyana na Yanga iliyoanza kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Tanzania Prisons, Septemba 6, Uwanja wa Mkapa


Said amesema:"Utakuwa mchezo wa kimbinu zaidi kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi. Imani yangu ni kwamba wachezaji wangu watakuwa tayari kwa ajili ya kupambana na kuweza kupata ushindi kwani ndicho ambacho tunahitaji.

"Mchezo wetu wa kwanza ilikuwa ni somo kwetu na kuona namna ambavyo tumefanya makosa. Ninaitambua Yanga na tutaingia ndani ya uwanja kwa kuwaheshimu wapinzani wetu, kikubwa mashabiki watupe sapoti," amesema.

Mbeya City, msimu uliopita ilipokutana na Yanga, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1. Hata ule mchezo wa mzunguko wa kwanza ambapo walikutana Uwanja wa Sokoine dakika 90 zilikamilika kwa sare ya bila kufungana.

Hivyo leo Septemba 13 itakuwa ni mchezo mkali kwa kila timu kusaka rekodi mpya ya kusepa na pointi tatu mazima.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic