September 13, 2020


 KOCHA wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic amesema ataanza kumtumia kiungo mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos katika michezo inayofuata ya ligi.

 

Carlinhos amesajiliwa na Yanga hivi karibuni akitokea nchini Angola, ameshindwa kupata nafasi ya kuanza katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa sare ya 1-1, Uwanja wa Mkapa, Septemba 6.

 

Kwenye mchezo huyo nyota huyo alikuwa benchi akipiga stori na myota mwenzake wa Rwanda, Haruna Niyonzima ambao wote waliishia kusugua benchi.


Krmpotic amesema Carlinhos ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ila bado hajawa tayari kucheza kutokana na kukosa utimamu wa mechi, lakini karibuni anatarajiwa kuwa fiti.


“Carlinhos ni mchezaji mzuri, tunatarajia kupata ufundi wake hivi karibuni lakini kwa sasa hajaonekana uwanjani kwa kuwa bado hana utimamu wa mwili katika kucheza mechi ila hivi karibuni ataonekana uwanjani.

 

“Ukiachana na yeye pia bado kuna wachezaji wengi ambao hawajawa fiti lakini tunatarajia kupata ubora wao huko mbeleni kwa kuwa wanahitaji muda kuonyesha ubora wao,” amesema kocha huyo.

 

Yanga inatarajia kumenyana na Mbeya City katika mchezo wao wa pili wa ligi, leo Septemba 13, katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.

2 COMMENTS:

  1. Hivi nyie waandishi mnashangaza Sana,wachezaji wote waliosajiliwa wanaweza kucheza mchezo mmoja?mechi bado nyingi atacheza Tu,msichoshe makocha kwa maswali ya ajabu

    ReplyDelete
  2. Kwa hiyo huyo carlinhos atakuwa fiti kwa kukaa benchi? Huyo kocha kamprotic hana tofauti na emayel-mzee wa manyani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic