September 25, 2020


 UONGOZI wa Polisi Tanzania umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC utakaopigwa kesho Septemba 26, Uwanja wa Ushirika, Moshi.


Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa kila kitu kipo sawa kuelekea mchezo huo kwa kuwa wachezaji wanatambua wajibu wao ni kusaka pointi tatu muhimu.

"Mchezaji mmoja atakosekana kwenye mchezo huo ni kipa Mohamed Yusuf yeye anasumbuliwa na majeraha ila wengine wapo vizuri.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuona namna tutakavyotoa burudani hasa ukizingatia tutakuwa nyumbani," amesema.

Polisi Tanzania inakutana na Dodoma FC iliyo nafasi ya nne na pointi zake saba baada ya kucheza mechi tatu. Polisi Tanzania ipo nafasi ya 9 na pointi 4.

Mechi ya Polisi Tanzania iliyopita ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Tanzania huku Dodoma FC ikilazimisha sare ya bila kufungana na Coastal Union, Mkwakwani, Tanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic