September 19, 2020

 


MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Zacharia Hans Poppe ameshangaa kuona hadi leo Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), haijampa barua ya hukumu yake ya kutakiwa kulipa faini ya milioni tano.

 

Hans Poppe, Msemaji wa Simba, Haji Manara na Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bombuli wamejikuta wakikumbwa na rungu la Kamati ya Maadili kwa kufanya makosa mbalimbali wakati wa hukumu ya Bernad Morrison.

 

Kwa upande wa Hans Poppe amekumbwa na adhabu hiyo kutokana na makosa mawili aliyoyafanya, moja likiwa ni kutoa taarifa ya shauri ambalo lilikuwa likisikilizwa huku yeye akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, pili kutoa maneno ya kiuchochezi kwa umma.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Hans Poppe amesema kuwa, anashangaa kuona hadi leo ‘juzi’ hajapatiwa barua ya hukumu yake na badala yake amekuwa akisikia masuala hayo kupitia wanahabari na kudai kuwa mara baada ya kuipata barua hiyo ataichambua na ili kujua kigezo kilichotumika.

 

“Bado hawajanipatia barua yoyote hadi sasa kutokana na maamuzi yaliyofanyika ya kupewa adhabu, siwezi kuchukua maamuzi yoyote, nimesikia maneno kutoka kwenu, wao walivyoniita awali kwenda kujieleza, walijua ni jinsi gani walinipata hadi nikaenda kwenye kile kikao chao na kutoa maelezo.

 

“Kwa nini wasinipe hukumu yao kupitia njia ileile ambayo waliitumia kuniita, kwa nini wasiniletee barua ya maamuzi waliyoyafanya na wanakaa kimya hadi leo au ni maneno tu yanatungwa.

 

“Nikiipata hiyo barua ndio nitajua vigezo gani vimetumika kunipa hukumu hiyo kwa sababu kama sijaridhika na maamuzi yao lazima nikate rufaa kwa sasa sielewi maelezo yao yakoje,” alisema Hans Poppe.

6 COMMENTS:

  1. Soka letu maigizo manara kalipa faini hanspoppe anasubili barua ya hukumu duh

    ReplyDelete
  2. Huyu msanii tu anajifanya kujitutumua tu ,anajua Karia yupo ,hata hizo adhabu ni elekezi Mtu yupo kwenye Kamati anakosa maadili alitakiwa afukuzwe pamoja na kulipa pesa lkn.Halafu huyu jamaa bness man mkubwa anang'ang'ania nini mpirani?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ameshakueleza vizuri kuwa hafahamu kuhusu hukumu hiyo imetolewa kivipi na alikosea nini na anahukumiwa kupitia kifungu gani cha kuhalilisha hukumu? Na yeye anasikia hukumu hiyo kupitia kwenye vyombo vya habari.Elewa kisheria anatakiwa apewe nakala ya hukumu ili ajiridhishe au akate rufaa asiporidhika.Kama ulivyodai kuwa huyu ni mfanyabiashara mkubwa hivyo uelewe kuwa wanakuwa na wanasheria wao ambao huwalipa na anapewa ushauri na mwongozo na sio kujiamulia yeye binafsi.Kutafisiri sheria sio jambo la kukurupuka kama wengi wetu tuanvyofikiria.Na hata unapokuwa na mashitaka mahakamani unashauriwa kuwa na wakili ili akusimamie ktk kukuogonza ktk kukabiliana na mashitaka uliyofungua au kufunguliwa wewe.Hivyo ni bora kukaa kimya kuliko kukurupuka na kumwita msanii wakati hufahamu kwa nini ametoa hilo jibu kwenye kamati ya maadili ya TFF.

      Delete
  3. Kwani gsm si ni wafanyabiashara wakubwa Sana kwani wanang'ang'ania mini kwenye mpira

    ReplyDelete
  4. Kwani huyo mwanasheria hakuwepo alivyoanza kukiuka maadili ya au hujui,Ukweli Ni kwamba hapa brother usituzuge mimi sijakurupuka ni kwamba tu mpira(soka)imekuwa sehemu ya Ubabaishaji cse mtu hawekwi ndani,mtu ashiriki kumshawishi mchezaji huyohuyo aende Kwenye Kamati ya kusuruhisha huyo huyo mara kwenye media kwa issue ile ile?hapa watu mnajua mnapenda Team zenu kaeni pembeni ,mnajishusha hadhi au naye anunue hisa Kama Mo hasa zile zinazo washinda mikia 51 percent cse hamna assets za thamani Hiyo.Mpira siyo uhadui na hizo kanuni mnajua hazipo lkn ilimradi kukomoana mmempata Morrison.Kwa Hiyo Haji Hana Mwanasheria?

    ReplyDelete
  5. GSM kawekekeza hayupo kwenye Kamati za Fitna TFF usimlinganishe na hao .Mpira utadhani tunawakilisha Bungeni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic