September 16, 2020


 PHARES Magesa, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania,(TBF) amewaomba wadau wa mpira wa kikapu waendelee kujitokeza kutoa sapoti katika maendeleo ya mpira huo.

 Magesa amesema kuwa maendeleo makubwa ya mpira wa kikapu ndani ya Tanzania yanahitaji sapoti kubwa kutoka kwa wadau na wanafamilia ya michezo.  

“Kikubwa tunahitaji kuona maendeleo katika kikapu na ili kuweza kufika malengo hayo tunahitaji sapoti kubwa kutoka kwa wadau na wanafamilia ya michezo ili kufikia malengo yetu," amesema.

Pia Magesa ameishukuru Serikali kwa kuwapa sapoti kwa kuwaboreshea na kuwajengea viwanja vipya vya mchezo wa kikapu na kuwaomba wadau waendelee kusapoti kikapu.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic