September 27, 2020


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong amewajibu mashabiki wa Simba kwa kuwaambia suala la yeye kushindwa kufunga haliwezi kumuumiza kichwa kwa kuwa anachokiangalia ni kuisidia timu yake kupata matokeo mazuri na ukifika muda wake watakosa la kuongea.

 

Sarpong amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sports ya Rwanda ambapo amefanikiwa kucheza mechi tatu za ligi huku akifunga bao moja pekee.

 

Mshambuliaji huyo amekuwa akibezwa mtandaoni na mashabiki wa Simba kutokana na kucheza mechi tatu katika ligi kuu msimu huu lakini amefanikiwa kufunga bao moja sawa na mshambualiji akipotezwa na Chris Mugalu wa Simba mwenye mabao mawili.


 Sarpong alisema kuwa suala la mashabiki wa Simba kumsema vibaya juu ya kushindwa kufunga haliwezi kumuumiza kichwa kwa kuwa muda ukifika wenyewe watakaa kimya kwani siku zote anatambua majukumu yake akiwa uwanjani.

 

“Siwezi kuumia wala kuchukia kwa sababu ya kufananishwa na mchezaji mwingine maana wanatakiwa kujua kwamba tunacheza kwenye timu mbili tofauti na wachezaji tofauti hivyo siwezi kuumizwa na hilo.

 

“Kitu kikubwa ninachokiangalia ni jinsi gani naweza kuwa msaada katika timu hilo ndiyo jambo muhimu kwa sababu tunahitaji kupata ushindi katika kila mchezo lakini wakati ukifika wao ndiyo watakaa kimya na hawatoamini kile ambacho kitatokea maana sipendi kuwa mtu wa mwisho," amesema.

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic