September 26, 2020

 


WINGA wa Yanga,Tuisila Kisinda amesema kuwa anajiona  bado hajacheza katika kiwango chake cha juu  lakini atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha anatoa mchango mkubwa kwa timu kuhakikisha inafanya vizuri katika michezo ijayo ya Ligi.


Yanga katika mchezo unaofuta wa ligi wanatarajiwa kumenyana na Mtibwa Sugar Jumapili, Septemba 27 katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kisinda amejiunga na Yanga akitokea Klabu ya AS Vita ya Congo ambapo tangia ajiunge na timu hiyo amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Yanga.

 Kisinda amesema kuwa bado hajacheza na kufikia katika kiwango chake cha juu  lakini atajitahidi kuhakikisha anatimiza majukumu ya Yanga kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya ligi kuu.

"Mashabiki wanatakiwa kuwa na subira lakini waendelee kuiunga mkono timu yao,kwa upande wangu  bado sijacheza katika kiwango kizuri lakini naamini  huko mbeleni kwenye michezo ijayo natarajia kuona mambo yakiwa mazuri.

“Kuhusu ligi ya Tanzania Kuna mambo najifunza kupitia ligi hii ambayo nimegundua kuwa inawachezaji wengi wazuri na ina ushindani mkubwa hivyo inahitaji kupambana ili kupata matokeo na mimi nipo tayari kwa hilo,” amesema Kisinda.

Kisinda kibindoni ana pasi moja ambayo aliitoa mbele ya Kagera  Sugar alimpa Tonombe Mukoko katika ushindi wa bao 1-0.

Kwa sasa timu ya Yanga ipo zake Morogoro ambapo ilitia timu jana kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kesho, Uwanja wa Jamhuri dhidi ya Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic