September 8, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa ulitambua mchezo wa kwanza wa ufunguzi dhidi ya Ihefu ungekuwa mgumu kutokana na mazingira ya miundombinu ya Mbeya kutokuwa rafiki hivyo wamejipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar. 


Septemba 6, Simba ilianza mbio za kutetea taji la Ligi Kuu Bara kwa kumenyana na Ihefu na ilishinda kwa mabao 2-1. Watupiaji kwa Simba ni John Bocco ambaye ni nahodha na Mzamiru Yassini huku lile la Ihefu likipachikwa na Omary Mponda.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji walipambana kusaka ushindi ila mambo yalikuwa magumu kutokana na  Uwanja wa Sokoine kutokuwa rafiki.


"Najua mashabiki wanatambua namna Simba inavyocheza hivyo kwenye viwanja vile ambavyo vina matatizo kidogo inakuwa ngumu kuona Simba yenyewe lakini mwisho wa siku tumeshinda na kupata pointi tatu hilo ni jambo muhimu kwetu. 


"Kwa sasa hesabu zetu ni kuelekea mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar,  utakuwa mchezo mgumu utakaochezwa wikiendi ila tupo tayari," amesema Manara. 


Mchezo huo utachezwa Septemba 12, Uwanja wa Jamhuri Morogoro ilipo ngome ya Mtibwa Sugar. Tayari Simba imeshawasili Dar, Septemba 7 kwa ajili ya kuanza kujiweka sawa kuelekea kwenye mchezo huo.


Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck inakwenda kukutana na Mtibwa Sugar inayonolewa na Zuber Katwila ambaye mchezo wake wa kwanza Septemba 6 alilazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Gairo.

7 COMMENTS:

  1. Bingwa si lazima acheze vizuri mechi zote, hizo ni dalili za bingwa.

    ReplyDelete
  2. Kikubwa ni ushindi. Kumbuka Timu imepanda daraja inabidi kujionyesha kuwa haijabahatisha kwa hiyo lazima ipigane kuonyesha siyo ya mchezo mchezo.

    ReplyDelete
  3. Kwani uwanja wa ccm kambarage ulikuwa mzuri? Sema tu walzidiwa uwezo na ihefu.na pia wamshukuru refa kwa kuwabeba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utopolo utawajua2 CCM kambarage Walchza na Tim gan au simba mech za lig kuu wamechza mbili aya tumekubal Yanga vs Prison Tim lenu bure kbsa

      Delete
  4. Uwanja wa CCM Kambarage alicheza nani tena?

    ReplyDelete
  5. Utopolo utawajua2 CCM kambarage Walchza na Tim gan au simba mech za lig kuu wamechza mbili aya tumekubal Yanga vs Prison Tim lenu bure kbsa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic