September 29, 2020

 




UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa ni muhimu mashabiki wake wakaelewa kwamba mpira sio uadui bali ni mwendelezo wa upendo na mshikamano katika kila jambo ambalo wanalifanya hivyo ni muhimu kwao kuacha kabisa tabia hiyo.


Septemba 27 wakati Yanga ikishinda bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, baadhi ya mashabiki wa Yanga walionekana kuleta vurugu jambo ambalo limekemewa vikali na Yanga wenyewe, Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) pamoja na wadau wa masuala ya mpira.


Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa kwa sasa elimu inaendelea kutolewa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mpira ili kuweza kuondoa kabisa tatizo hilo.

"Mashabiki wa Yanga wanapaswa waelewe kwamba mpira sio uaduia ni furaha na mshikamano, kwa sasa elimu inazidi kuendelea kutolewa lengo ikiwa ni kupunguza na kuondoa kabisa hili tatizo.


"Kwa mashabiki wa Simba, Yanga sisi sio maadui bali tunafanya ule utani wa jadi, jukumu ni letu pia tuna kazi ya kufanya kama ilivyokuwa zamani ambapo utani ulikuwa ni kwenye mpira pekee ila upendo unadumu huku kwenye shida wakiwa pamoja ikiwa ni kwenye misiba hivyo muhimu kuendeleza utamaduni," amesema.

6 COMMENTS:

  1. Mmepanda mbegu za chuki sasa mnajitia kuhangaika kiuongo. Mlizidi kuwadanganya mashabiki wenu kuwa wanaonewa ili kuficha ukweli kwamba timu yenu ilikuwa dhaifu sasa matunda mnayaona. Fujo zimehamasishwa na hao hao viongozi wa yanga. Ni aibu sana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesahau chuki anazoeneza mfalme wenu haji manara?

      Delete
    2. This comment has been removed by the author.

      Delete
    3. UnknownSeptember 29, 2020 at 7:10 AM we ni rafiki yake mkubwa James Delicious kwani jana nilikuona ukienda kumlaki akitokes segerea!

      Delete
  2. Hao wamezowea uhuni, kupiga, kuchana nguo za waungwana na kuzomea kwasababu bado hawajaonja rungu la TFF, kinyume na Simba jisi kulivopowa na nawapa hongera jinsi Namna walivostaarabika na jinsi Wanavoipenda a na kushuukuru neema zinavowaingilia na kila wanaposhinda juu ya kiwango walokuwanacho mara wale wapiga watu husema Hao wameuziwa mechi

    ReplyDelete
  3. Kihelehele chenu mechi sio yenu mnasafiri mpaka Moro kuloga mtapigwa sana mwaka huu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic