October 28, 2020

 


THABIT Zakaria, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa walipaswa kufungwa na Mtibwa Sugar ili kuondoa presha kwa wachezaji ambao walikuwa wanapambana kutunza rekodi ya kucheza mechi zao zote bila kufungwa.

Azam FC ilikuwa imecheza mechi saba bila kupoteza na safu yake ya ushambuliaji imetupia mabao 14 na ilikuwa imefungwa mabao mawili rekodi hiyo ilitibuliwa na Mtibwa Sugar ambao walishinda bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Oktoba 26.    

Thabit amesema kuwa kufungwa kwao ni kengele ya tahadhari ambayo itawafanya waongeze juhudi kwenye mechi zao zijazo ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

“Tulicheza bila kupoteza mechi saba ila naona ni jambo jema kwa kuwa wachezaji walisema kuwa wanacheza kwa presha kulinda rekodi. Ila kwa sasa ni furaha kuwa hatutakuwa na presha kwenye mechi zinazofuata, ilikuwa zamu yetu kufungwa na tumewaonesha Watanzania kwamba tunaweza kufungwa na pia tunaweza kushinda.

“Mtibwa Sugar walikuwa wanapambana na vitu viwili kwanza kupata pointi tatu na kuwa wa kwanza kuifunga timu ambayo haijafungwa, wapinzani wetu walicheza vizuri.Nasi pia tulicheza vizuri ila ilikuwa bahati mbaya kwetu.Tunarudi nyumbani tutaendelea kupambana,” amesema Thabit.

Mchezo wake unaofuata Azam FC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 21 itamenyana na JKT Tanzania Uwanja wa Azam Complex, Novemba Mosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic