October 16, 2020


KOCHA mpya wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze amemtaja aliyekuwa beki wa Yanga, Kelvin Yondani kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wenye heshima kubwa kwake na alitamani kufanya naye kazi ndani ya timu hiyo.

 

Kocha huyo aliwasili jana usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM) akitokea nchini Canada tayari kwa kuanza majukumu mapya ndani ya timu hiyo akichukua nafasi ya Mserbia, Zlatko Krmpotic aliyetimuliwa kutokana na mwenendo mdogo wa timu hiyo licha ya matokeo ya ushindi kwenye mechi zake.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaze alisema kuwa amewafuatilia wachezaji wote wa timu hiyo huku akimtaja Yondani kama ni mmoja wa mabeki bora na mwenye nidhamu ambaye alitamani kufanya naye kazi.

 

“Nimefuatilia wachezaji Yanga ambao walikuwepo tangu awali hata akina Juma Abdul ambao wameondoka pamoja na nahodha Kelvin Yondani wengine wakiwa akina Deus Kaseke, Juma Mahadhi, Fei toto, Ramadhani Kabwili, akina Metacha Mnata, nimewafuatilia wote wa Yanga wanafika 50.


"Yondani ni mchezaji mzuri ambaye amefanya mambo makubwa ndani ya Yanga.Natumia fursa hii kumshukuru kabisa hata rafiki yake akisikia amwambie mwalimu Kaze, anashukuru mchango wake ndani ya Yanga.


"Najua kila kitu katika maisha huwa na mwanzo na mwisho wake, kitu ambacho anapaswa kutambua ni kwamba yeye ni mchezaji mwenye nidhamu kubwa kwenye timu yetu, nilitamani angekuwepo lakini ndiyo hivyo mambo hayakwenda sawa,” alisema Kaze.

4 COMMENTS:

  1. Yondoni kauza mechi zetu nyingi sana. Kocha asituchanganye, yeye afanye kazi yake iliyomleta.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli kabisa, Kaze aache kututajia hilo jina kama anataka kuendelea kuheshimika klabuni. Huyo mtu hatutaki hata kumsikia. Wameuza mechi zetu nyingi na mikia, sisi mashabiki tunaumia wao baada ya mechi wanaenda kunywa bia.

      Delete
    2. Ahahahahaaaaaaaaa ni kweli mpo sahihi kabisa waacheni waende namongo hkohko walichotufanyiaga hao mafyatu sintakaaa kusahau na endapo yondan,juma abdul,papy, na morrison wataludi jangwan basi ndo siku hyohyo naachana na yanga

      Delete
  2. Ni kweli nakuunga mkono kaze coz Yondani haikupaswa wamuachie aondoke kutokana na uzalendo aliokuwa akiuonyesha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic