NYOTA wa Simba kiungo Gerson Fraga na nahodha John Bocco wapo Kwenye uangalizi maalumu ndani ya kikosi hicho ili Kurejea Kwenye ubora wao.
Fraga aliumia nyonga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United na nahodha Bocco naye pia aliumia akiwa na Simba Kwenye mechi za Ligi Kuu Bara jambo lililomfanya Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amuondoe Kwenye timu ya Taifa ambayo ilikuwa inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi.
Mchezo huo ulichezwa Oktoba 11 na Stars kukubali kichapo cha bao 1-0 dakika za usiku jambo lililoyeyusha furaha kwa mashabiki wa Stars.
Simba baada ya kumaliza mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania walikuwa mapumziko ya siku tatu na kwa sasa tayari wamesharejea kambini. Jana Oktoba 13 walipaswa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ndanda ila hali ya hewa ya mvua ilitibua mambo.
Patrick Rweyemamu, meneja wa Simba amesema kuwa tayari kwa sasa kikosi kipo kambini kikiwa kimeanza maandalizi ya mechi zijazo.
"Kikosi kipo kambini kwa sasa kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo baada ya mapumziko mafupi ya siku tatu baada ya kumaliza mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Dodoma.
"Kwa upande wa mazoezi ambayo tulianza nayo awali ilikuwa ni pamoja na Gym kwa wachezaji wote ambao hawajasafiri kwenda kwenye timu zao za Taifa kwa ajili ya mechi za kimataifa lakini wachezaji wetu John Bocco na Gerson Fraga bado wapo Kwenye uangalizi maalumu kutokana na majeraha wanayouguza," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment