October 14, 2020

 


CEDRIC Kaze anayetajwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao anatambua kwa undani uwezo wake ni pamoja na kiungo Muangola wa timu hiyo Carlos Carlinhos.


Carlinhos ni namba moja ndani ya Yanga kwa kutengeneza pasi za mwisho na mpigaji wa mipira iliyokufa ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapendwa na mashabiki kutokana na kasi yake ndani ya Uwanja.


Yanga ikiwa imefunga mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara amehusika kwenye mabao matatu akifunga bao moja na kutengeneza pasi tatu za mabao na yote yalifungwa na Lamine Moro. 


Akizungumza na Saleh Jembe,  Kaze amesema kuwa anamtambua vema Carinhos na anajua kwamba ni mchezaji mzuri ambaye akiyazoea mazingira atakuwa na hatari ndani ya uwanja.


"Ujue yule Carlinhos namtambua muda mrefu na ni mchezaji mzuri ambaye ana uwezo mkubwa ndani ya uwanja kwa namna ambavyo anafanya nina uhakika kwamba atakuja kuwa bora wakati ujao na atakuwa na hatari kubwa akiwa kazini.


"Nimemuona ni mzuri kwenye kuchezesha timu na kupandisha mashambulizi, mipira iliyokufa imekuwa ni hatari kwake hivyo akiweza kuendana na mazingira ya Bongo basi Yanga watarajie makubwa kutoka kwake, " amesema. 


Kaze ambaye anatajwa kuja kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi Oktoba 3 anatarajiwa kutua Bongo kesho Oktoba 15 akitokea Canada ambapo yupo kwa sasa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic