JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakifanya makosa ambayo yanajirudia jambo ambalo linamfanya akose raha kila mara pale wanapopoteza.
Jana, Oktoba 3, Coastal Union ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mgunda amesema kuwa imekuwa ni kawaida kwa wachezaji wake kupoteza kwa kufanya makosa yanayojirudia jambo linalomfaya afikirie namna mpya ya kutatua matatizo hayo.
"Wachezaji wangu wapo vizuri na uwezo wanao ila tatizo lao ni kwamba wanafanya makosa ambayo yanajirudia jambo ambalo linaniumiza pia.
"Nikiwa kwenye benchi na nikiwa mwenye majukumu ya kuwasimamia ninatumia nguvu kubwa kwenye kuongea nao na mpaka wakati mwingine sauti yangu inapotea kabisa," amesema.
Coastal Union kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 4 baada ya kucheza mechi 5 huku ikipoteza tatu, sare moja na kushinda mechi moja na Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 13.
Mtakesha Sana kupata matokeo against Simba na Yanga CSE nimeona wengi mnakuwa na game plan moja tu na mala nyingi mnashindwa kwenye sub
ReplyDeletesorry MrMgunda kwa Team na aina ya Wachezaji ulo nao na hadhi yao,sema Mungu akhasante ninastahili kupata hv inatosha.Hata bila makosa Wachezaji wako wanaonyesha uwezo wao.