October 4, 2020



UWANJA WA Sukru Saracoglu ni miongoni mwa ule wa mwanzo kabisa kutikiswa na nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta kwa kuwa alitikisa nyavu mara mbili akiwa na timu yake mpya.
Samattta alitupia kwenye ushindi wa mabao 2-1 kwa timu yake ya Fenerbahce aliyojiunga nayo kwa mkopo akitokea Klabu ya Aston Villa ya England dhidi ya Faith Karagumruk kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki.
Nyota huyo mwenye miaka 27 ni mechi yake ya kwanza kuanza kikosi cha kwanza ambapo ile ya kwanza alianzia benchi.

Alitupia mabao hayo dakika ya 24 kwa pasi ya Caner Erkin na alipachika bao la pili dakika ya 68.Hakuyeyusha dakika zote 90 alitumia jumla ya dakika 84.

Mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Galatasaray wiki iliyopita ambapo alicheza kwa dakika 25 mechi ikimalizika kwa suluhu.


3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic