October 12, 2020


 IMEELEZWA kuwa, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze raia wa Burundi, tayari ameanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kwa kutuma programu zake kwa kocha msaidizi, Juma Mwambusi.

 

Kaze ambaye ameshafikia makubaliano na Yanga kuinoa timu hiyo akichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic raia wa Serbia aliyetimuliwa hivi karibuni, anasubiriwa kutua tu ambapo taarifa kutoka Yanga zinasema kwamba, Alhamisi ijayo ya Oktoba 15, mwaka huu atakuwa katika ardhi ya Tanzania akitokea Canada.

 

Chanzo kutoka katika benchi la ufundi la Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Mara kwa mara Kaze anawasiliana na Mwambusi ili kufahamu kikosi kinaendeleaje, amekuwa akituma program anazotaka wachezaji wapatiwe na Mwambusi anazifanyia kazi.

 

“Hata mechi ya kirafiki ambayo Yanga imecheza dhidi ya Mwadui yeye ndiye amependekeza, pia amekuwa akiwafuatilia wachezaji katika mechi za nyuma kupitia video za mechi zao.”


Kwa sasa Yanga ipo chini ya Mwambusi tangu Oktoba 3 baada ya Zlatko kufutwa kazi ndani ya Yanga.

2 COMMENTS:

  1. waandishi wanatafuta cha kuandika front page ili kuuza magazeti..

    hakuna siku gazet hili likapita bila kueleza habar za kocha yanga, au habari za yanga, je ni kweli mwandishi anawasiliana kila siku na uongozi wa yanga?
    hatupend uongo, kama huna habari si lazima kuandika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic