NYOTA wa kikosi cha Simba 11 walioitwa timu zao za Taifa wamehusika kwenye mabao 14 yaliyofungwa na timu hiyo kati ya mabao 14 ambayo yamefungwa kwenye mechi tano.
Oktoba 18 walikuwa na kibarua cha kucheza na watani zao wa jadi Yanga ila mchezo huo umepelekwa mbele na Bodi ya Ligi Tanzania utachezwa Novemba 7.
Wachezaji wa Simba walioitwa kwenye timu zao za taifa ni pamoja
na Luis Miqiussone mwenye pasi tano za mabao na ana bao moja kibindoni
ameitwa timu ya Taifa ya Msumbiji.
Clatous Chama raia wa Zambia amefunga mabao mawili na ana pasi
tatu za mabao ameitwa timu ya Taifa ya Zambia. Francis Kahata wa Kenya
yeye ni kiungo na Joash Onyango wa Uganda yeye ni beki ametumia dakika 450
uwanjani kwenye ligi na timu yake imefungwa mabao mawili.
Kwa wazawa ni Mzamiru Yassin kiungo mkabaji amefunga mabao mawili na ana pasi moja ya bao huku nahodha John Bocco akiwa amefunga bao moja kwenye ligi.
Aishi Manula yeye ni kipa ametumia dakika 450 uwanjani na
amefungwa mabao mawili akiwa na ‘cleansheet’ tatu kwenye mechi tano.
Shomari Kapombe
ameyeyusha dakika 450 kwenye mechi tano za ligi sawa na nahodha msaidizi
Mohamed Hussein.Said Ndemla yeye ni kiungo ametumia jumla ya dakika 181 kati ya
450 huku Jonas Mkude uwezo wake na uzoefu ukimbeba.
0 COMMENTS:
Post a Comment