October 9, 2020

 


WAKATI mashabiki wa Yanga wakimsubiria kwa hamu kubwa kocha mpya wa timu hiyo, Cedric Kaze raia wa Burundi, imebainika kuwa kocha huyo ndiye aliyehusika na usajili wa nyota wa kikosi hicho waliosajiliwa hivi karibuni katika dirisha lililofungwa Agosti 31, mwaka huu.

 

Yanga ipo katika hatua za mwisho za kumtambulisha Kaze kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho baada ya kuachana na Zlatko Krmpotic raia Serbia.


Ikumbukwe kuwa, kabla ya Zlatko hajapewa nafasi ya kuinoa Yanga, uongozi wa timu hiyo ulifanya mazungumzo na Kaze ambaye dakika za mwisho akapata udhuru, akashindwa kujiunga na timu hiyo.

 

Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, Kaze akahusika kufanya usajili wa nyota wa kikosi hicho akiwemo Tonombe Mukoko, Tuisila Kisinda, Songne Yacouba, Michael Sarpong, huku akihusika pia kumleta kocha wa makipa, Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi.

 

Taarifa ambazo Spoti Xtra imezipata kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, Kaze anatua Yanga akiwa kamili kwa kuwa kikosi kilichopo anahusika nacho kwa asilimia zote kutokana na kusajili baadhi ya nyota wa kimataifa, hivyo ataweza kuwatumia tofauti na ilivyokuwa kwa Zlatko.

 

“Uongozi unaendelea na mazungumzo ya mwisho na kocha Kaze ambaye atatua wakati wowote kuanzia sasa baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia na kila mmoja ana matumaini makubwa na kocha huyu kwa kuwa ni mtu wa kazi, hivyo atakuja kuipa ubingwa Yanga.


"Kaze anatua Yanga akiwa kajiandaa kwani asilimia kubwa ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu yeye anahusika kwa kiasi kikubwa kwani nyota kama Kisinda, Mukoko, Yacouba na Sarpong wote amewasajili yeye pamoja na kocha wa makipa ambaye ni chaguo lake.

 

“Amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na kikosi, hivyo ni kocha ambaye anakijua vyema kikosi cha Yanga kuliko kocha aliyeondoka ambaye alikuwa hakijui vizuri kikosi.


“Watu wanatakiwa kuelewa kwamba, Zlatko kilichomuondoa zaidi ni kushindwa kuwatumia vizuri wale wachezaji ambao kwa kiasi kikubwa hakuhusika kwenye usajili, lakini huyu Kaze atafanya vizuri,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alipoulizwa juu ya ujio wa kocha huyo alisema: “Wakati wowote kuanzia sasa kocha atatua na kuanza kazi mara moja.”


3 COMMENTS:

  1. Hata Zahera nae si alifanya hayohayo na makubwa kuliko hayo mara Mia, lakini tuliuona mwisho wake wa kunyolewa nyewle kavukavu Bila ya kurowekwa kwa sabuni

    ReplyDelete
  2. Zahera alisanili team nzima yy mwenyewe yakamshinda sasa ndo hiki kiazi chenu zamu yake imewadia

    ReplyDelete
  3. Zahera alisanili team nzima yy mwenyewe yakamshinda sasa ndo hiki kiazi chenu zamu yake imewadia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic