October 28, 2020


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa bado hajajua sababu ya kupoteza mechi mbili mfululizo jambo ambalo linampa tabu katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.


Wakiwa ni mabingwa watetezi wameyeyusha jumla ya pointi nane ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 baada ya kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na ilipoteza mechi mbili ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 na mbele ya Ruvu Shooting kwa kufungwa bao 1-0.


Timu zilizompa tabu Sven ni zile za majeshi ambazo muda wote wapo fiti asilimia 100 kwa kuwa kazi yao ni mazoezi, Tanzania Prisons na Ruvu Shooting.

Ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi saba za ligi kwa msimu wa 2020/21.


"Matokeo mabaya na hayafurahishi ila bado sijajua sababu ni ipi katika kupoteza mechi zetu, ile ya kwanza ilikuwa ni sehemu ya mchezo naona imejirudia tena mbele ya Ruvu Shooting.


"Bado hatujakata tamaa tuna amini kwamba tutarejea kwenye ubora wetu na tutafanya vizuri katika mechi zetu zijazo," amesema.


Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Oktoba 31.

4 COMMENTS:

  1. Kama bado hujui ubingwa basi tena

    ReplyDelete
  2. Haha anatakiwa ajue ili apate ufumbuzi, au atazame upana WA hicho kikosi kimapanukaje

    ReplyDelete
  3. Kocha simba aliwaamini wachezaji wake wakamuangusha ndio maana anashindwa kufahamu vipi amepoteza mechi zile kizembe. Watanzania wanampenda John ila kwangu mimi simkubali hata kidogo na nina sababu zangu.Kwanza kwenye big match iwe ya taifa au ya Klabu ambayo inahitaji mchezaji mkubwa kufanya mambo makubwa siku hiyo ndio Boko anaiangusha timu. Pili Boko ni muoga wa kwenda kuingiana maungoni na beki hasa beki wa kati. Tatu kwa kitambo tu sasa Boko licha ya majeruhi lakini anaonekana kupoteza umakini na utumivu katika suala la umaliziaji. Tuwe wa kweli kwa miaka sasa watanzania tumeshindwa kuzalisha wachezaji wenye kuamua mechi kubwa hata huyo Samata kwenye timu ya taifa uwezo wake ni tia maji tia maji. Yaani nazungumzia wachezaji tuliowasikia huko nyuma wa kitanzania wakifanya mambo mazuri ya kushangaza uwanjani bila ya kujali wanacheza na nani au timu gani. Mchezaji kama Zamoyoni Mogela, peter Tino,Ntenze John,Mohanedi Husein Mmachinga na wengine kadhaa hawa ni wachezaji ambao ilikuwa ukibeti kuwa watafanya mambo makubwa kwenye mechi kubwa basi kweli watafanya makubwa.Mfano mzuri pale simba ni cletus chama wa Zambia ukimtegemea kufanya mambo makubwa kwenye mechi kubwa kweli anafanya makubwa. Wachezaji wazawa pale simba wajitafakari kwani simba hii ndio tunayoitagemea kwenda klabu bingwa Africa.Na sio Sven hata Matola ajitafakari kwani mechi kama hizi za wanajeshi zenye wachezaji asilimia mia moja wazawa yeye matola ndie mwenye ufahamu mzuri zaidi wa kumshauri kocha wake.kiukweli wachezaji wa simba wapo legelege sana kama wadada vile.

    ReplyDelete
  4. Wachezaji WA simba hasa wazawa wamekuwa magoigoi hawakazi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic