October 28, 2020

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Simba imewafuta kazi Mwarami Mohamed (Kocha wa magolikipa) na Patrick Rweyemamu (Meneja wa timu ) kutokana na matokeo mabaya kwa mechi mbili  Mfululizo 

Simba imecheza mechi mbili mfululizo na kupoteza pointi sita ambapo ilianza kufungwa bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ikachapwa tena bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.


Kwenye mechi mbili ambazo zilikuwa zinahusisha timu za majeshi wenye mwendo wa kucheza ligwaride, Simba imeyeyusha pointi sita na kufungwa mabao mawili.

Pia inaelezwa kuwa wangine ambao wamefutwa kazi ni Ally Shatry ‘Bob Chico’ na  Jacob ambao  walikuwa kwenye  kitengo cha Habari cha Klabu hiyo.


Wawili hao wamefutwa kazi  kwa kile kinachosadikika kuwa karibu na CEO wa zamani Senzo Mazingiza ambae hivi sasa yupo Yanga.


Patrick Rweyemamu ambaye anatajwa kufutwa kazi hakuwa tayari kuzungumzia hilo pamoja na Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe.

16 COMMENTS:

  1. Aisee haya ndio vilabu vyetu hivi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu Muharami simba walitakiwa kumfukuza kazi siku nyingi. Alipaswa kufukuzwa wakati ule mzee wa Uchebe alipotumbuliwa. Manula ameendelea kurejea makosa yale kwa yale kila mara kama vile hana kocha. Mbaya zaidi Beno kakolanya nae ameshuka kiwango na anafanya makosa yale kwa yale sasa kama manula. Unakumbuka hamsa 5 hamsa 5 za klabu bingwa Africa basi mpaka leo manula hajajifunza kitu bado kwenye yale makosa.So far uongozi wa simba haujatuangusha kwenye maamuzi haya sijui hapo baadae kwani simba hawatakiwi kumfukuza kazi kocha wao wa sasa ni kocha mzuri kama atapata wasaidizi makini. Kitu kimoja simba wanatakiwa kumshauri kocha wao ni kutafuta kocha wa mabeki kwani ndio silaha kubwa ya kufanya vizuri klabu bingwa Africa. Ukiweza kuzuia usifungwe kirahisi ugenini kwenye klabu bingwa Africa basi utafika mbali. simba wanatakiwa kukomaa zaidi kwenye kuimarisha beki yao ikiwezekana wamuandae Ame kucheza Diffence midfield ili kuongeza zege kwenye kisiki.

      Delete
  2. Wafukuze aliyewasadikisha kuwa wana kikosi kipana.....

    ReplyDelete
  3. Kwani hawa wapo bench la ufundi?

    ReplyDelete
  4. Baada ya mechi niliona mbishano mkubwa baina ya Matola na Kakolanya, ikielekea Matola alitaka kumlaumu Beno, Beno akamtolea uvivu!

    ReplyDelete
  5. Eti hao ndo watavuka kuingia makundi thubutuuuuu, kama mnahenyeshwa na hizi timu zinazoonekana za kawaida huo moto Wa Ahly aunt Esperance mtauweza kweli kama si kuendelea kunyukwa 5G tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Walikuja Al Ahly hapa mkasema wana mchezaji ana thamani ya bilioni kumi simba hawewezi kuifunga Al Alhy kilichotokea wake zetu walienda kulala mapema leo tena wake zetu(Utopolo) wanarudia maneno yaleyale, sasa si muhamie tu huko Al Ahly tujue sasa hv wake zetu(Utopolo) ni washabiki wa Al Ahly

      Delete
  6. Angefukuzwa na huyo kocha na benchi lote ujinga mtupu hapo na bado tutafungwa kila mechi

    ReplyDelete
  7. Mashabiki wa Yanga mna shida gani? Kafungwa Simba nyie mnaongea sana juu ya timu hiyo, kwani wameomba ushauri wenu? Angalieni timu yenu jamani.

    ReplyDelete
  8. Kiukweli simba ilibidi iwape mda zaidi benchi la ufundi hebu tuangalie wenzetu tunakaribia kanza kwa michuano ya kimataifa kwa kufanya hivyo wataharibu mipangilio ya timu kiufundi

    ReplyDelete
  9. Kiukweli simba ilibidi iwape mda zaidi benchi la ufundi hebu tuangalie wenzetu tunakaribia kanza kwa michuano ya kimataifa kwa kufanya hivyo wataharibu mipangilio ya timu kiufundi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh muda gani tena wapewe?.. November ndio hiyo imeshaingia na klabu bingwa ya Africa inaanza.Ukweli timu yetu ya Simba inacheza mpira laini na kwenye mashindano haya naona hadithi itajirudia ya UD Songo.

      Delete
  10. Kweli kabisa simba inacheza kilaini laini taff game Ni shida.

    ReplyDelete
  11. Makosa mengine ni yawachezaji, kuwatimua banchi la ufundi ni kuwaonea, makosa ya Manula yanajirudia rudia inaonekana ni kasoro zake za kibinadamu lkn coach ahusiki hata aje nani atafanya hivyohivyo kwasababu kubadilika ipo nje ya uwezo wake, na ndio ubinadamu wenyewe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic