VITA ya kupanda Ligi Kuu Bara ikiwa imeanza kwa timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, raundi ya kwanza imeweka rekodi kwa kukusanya jumla ya kadi 27 za njano kwa wachezaji huku moja ikiwa ni nyekundu.
Kwenye makundi mawili yaLigi Daraja la Kwanza ambayo ni A na B yakiwa na jumla ya timu 20 na kila kundi lina timu 10, kundi B limetia fora kwa kukusanya kadi nyingi za njano ambazo ni 20 huku kundi A likiwa na kadi 7 za njano.
Waliopata kadi za njano mzunguko wa kwanza ni :-Oscar Mwambinga na Kassim Juma wa African Lyon. Isaya Mwaka wa Boma FC. Gerald Edward, Kashiru Salum na Mashaka Issa wa Majimaji pamoja na Yassin Saleh huyu ni mali ya Njombe Mji.
Kundi A mzunguko wa kwanza zilikusanywa jumla ya kadi 7 za njano na timu iliyokusanya kadi nyingi za njano ni Majimaji ya Songea ambayo ilikusanya tatu ikifuatiwa na African Lyon ambayo ilikusanya kadi mbili za njano.
Kundi B ndilo lina balaa zilikusanywa jumla ya kadi 20 za njano na AFC walitia fora kwa kuonyeshwa kadi sita za njano ikifuatiwa na Klabu ya Singida United ambapo wachezaji wake wanne walionyeshwa kadi za njano na kwa upande wa Mbao FC wachezaji wake watatu walionyeshwa kadi za njano.
Ally Bakari wa Alliance FC. Ezekiel Robert, Muntala Yusuf, Yella Mboma, Omary Wazir, James Zamba, Miraj Ibrahim hawa ni wa AFC. Faisal Mganga na Emmanuel Mwita ni wa Kitoyasce FC.
Elia Elia, Aman Juma na Alex Mwaisaka hawa ni wa Mbao FC. James Shangala wa Pamba FC. Nkuba Clement na Kenani Kasea wa Rhino Rangers. Shaban Seif, Simon John, Anjero Mbilinyi na Erick Mambo hawa ni wa Singida United.
Kadi nyekundu kwa mzunguko wa kwanza ilipatikana moja ilikuwa ni kwa Alex Mwaisaka wa Mbao FC alionyeshwa kadi mbili za njano na aliukosa mchezo dhidi ya Kitoyosce FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment