October 6, 2020

 


UONGOZI wa Klabu ya Ihefu yenye maskani yake Mbeya, leo Oktoba 6 imetangaza kusitiksha mkataba wa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Maka Mwalwisi.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Uongozi wa Ihefu haijaeleza sababu za kuachana na kocha huyo.

Anakuwa ni kocha wa pili kufutwa kazi ndani ya Oktoba baada ya Yanga kuanza kufanya hivyo Oktoba 3 kwa kumfuta kazi Zlatko Krmpotic. 

Ihefu imekuwa kwenye mwenendo mbovu ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni msimu wake wa kwanza kushiriki ligi baada ya kupanda msimu huu kutoka Ligi Daraja la Kwanza.


Mchezo wake wa kwanza kucheza Septemba 6 ilitunguliwa mabao 2-1 na Simba na ilishinda mchezo mmoja mbele ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar.


Ilipoteza mchezo mwingine mbele ya Mwadui FC kwa kufungwa mabao 2-0 na imepoteza mchezo wake wa raundi ya tano kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Ihefu jambo ambalo linaonyesha wamekuwa kwenye mwenendo mgumu.


Kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 kibindoni ina pointi tatu imefungwa mabao saba na imefunga mabao mawili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic