PICHANI Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiwa na tuzo na cheti cha heshima cha kutambua mchango wa ushirikiano baina Global Publisher ambao ni wachapishaji wa magazeti ya michezo ya Championi na Spoti Xtra.
Global walikabidhiwa tuzo na cheti hicho kutoka Vodacom katika sherehe ya maadhimisho ya miaka 20 ya utoaji huduma bora nchini Tanzania iliyofanyika leo Jumanne katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Aidha, Vodacom pia walizindua kampeni mpya ya ‘Pamoja Tuyajenge Yajayo’ .
Tuzo na cheti hicho vilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Vodacom, Hisham Hendi ambaye pia alitoa hotuba ya tulipotoka, tulipo, na tunapokwenda kuhusu huduma za Vodacom.
0 COMMENTS:
Post a Comment