LIGI kuu ya soka nchini England inarejea tena wikiendi hii baada ya mapumnziko mafupi kupisha mechi mbalimbali za kimataifa macho na masikio ya wengi yatakuwa katika jiji la Liverpool kwenye dabi maarufu kama Merseyside, ambapo Everton watawakaribisha mabingwa watetezi wa EPL na majirani zao, Liverpool.
Mechi hii inatajwa kuwa kali kuwahi kutokea kutokana na timu ya Everton kujiimarisha vizuri kwenye kikosi chao ambacho kinaongoza msimamo wa ligi na pointi 12 wakishinda mechi zote nne, huku upande wa Liverpool wakianza vibaya msimu huu baada ya kumbukumbu ya kufungwa kwa kipigo cha aibu cha mabao 7-2 dhidi ya Aston Villa kabla mapunziko ya mechi za kimataifa.
Katika miaka ya hivi karibuni majogoo wa jiji wamekuwa wakiiadhibu Everton lakini mechi ya leo ni ngumu na inaonekana karata kuangukia upande wa vijana wa Carlo Anchelotti, wakiongozwa na fowadi aliyepo kwenye kiwango bora kabisa, Dominic Calvert Lewin, mwenye magoli sita na uwepo wa kiungo mshambuliaji, James Rodriguez, aliyesajiliwa kutoka Real Madrid.
Safu ya ushambuliaji ya Liverpool ikiongozwa na Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Fermino siyo ya kubeza, ila upande wa ulinzi ndiyo unatia mashaka na huenda matokeo ya mechi hii ikaamuliwa na safu itakayokuwa bora kwenye ulinzi. Mechi itakuwa ya mapema kabisa ikichezwa mishale ya saa nane mchana kwa saa za Afrika Mashariki
Mechi zingine kali ni kati ya Chelsea dhidi ya Watakatifu wa St. Mary, Southampton, Newcastle watambana na Manchester United na mechi ya kufungia siku ni kati ya Mwalimu Pep Guadiola dhidi ya mwanafunzi wake, Mikael Arteta, yaani Manchester City watakwaana na Arsenal.
0 COMMENTS:
Post a Comment