October 29, 2020

 


ZIMEBAKI siku tisa kwa sasa kabla ya dabi ya Yanga na Simba ambayo inatarajiwa kuchezwa Novemba 7, Uwanja wa Uhuru, tayari Cedric Kaze Kocha Mkuu wa Yanga na Sven Vandenbroeck Kocha Mkuu wa Simba wameanza kuandaa mitambo yao ya kazi.

Yanga ambao ni wenyeji kwa sasa wanajiandaa na mchezo dhidi ya Biashara United utakaochezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 31 na Simba wao wanajiandaa na mchezo dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 31.

Tayari Kaze ambaye ni kocha mpya aliyesaini dili la miaka miwili akichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic amekiongoza kikosi chake kwenye mechi mbili ambazo ni dakika 180 ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru wakati akishinda bao 1-0 na ule wa pili wakati akishinda mabao 2-1 dhidi ya KMC Uwanja wa Kirumba.

Sven yeye baada ya Kaze kutua Bongo amekiongoza kikosi kwenye mechi mbili na zote amechezeshwa gwaride mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ule dhidi ya Ruvu Shooting zote alipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Majembe ambayo yamepewa nafasi kwa mechi za Kaze ni Metacha Mnata ambaye ni kipa ametumia dakika 180 na amefungwa bao moja huku Sven kichwa kikimpasuka kwa kuwa makipa wote wawili majanga, Aishi Manula alitunguliwa bao moja mbele ya Prisons na Beno Kakolanya alitunguliwa bao moja mbele ya Ruvu Shooting.

Kwenye safu ya ushambuliaji, Wazir Junior ametumia dakika 81 na amefunga bao moja mbele ya KMC wakati Yanga ikifunga jumla ya mabao matatu kwenye mechi mbili kwa Simba hakuna mshambuliaji aliyefunga ndani ya dakika 180.

Viungo wa Yanga, Tuisila Kisinda ni mtambo wa mabao ndani ya Yanga na pacha wake Tunombe Mukoko wote wamefunga bao mojamoja chini ya Kaze. 

Farid Mussa ameonekana kuwa bora kwa kutengeneza pasi za mwisho akiwa nazo mbili na ametumia dakika 108 uwanjani.

Simba hakuna kiungo kwenye mechi hizi mbili ambaye amefunga walakutengeneza nafasi,kiungo aliyetumia dakika nyingi ni Jonas Mkude ameyeyusha dakika 180 na Luis Miquissone.

Kwa upande wa mabeki, Kaze anawaandaa Bakari Mwamnyeto na Lamine Moro ambao wameyusha dakika 180 na wamefungwa bao moja huku Sven akiwaandaa Joash Onyango, Mohamed Hussein na Shomari Kapombe ambao wameyeyusha dakika 180 na wameshuhudia makipa wao wakiokota mabao mawili.


Clatous Chama kiungo wa Simba yeye mechi mbili ambapo Simba imepoteza alikosekana kikosi cha kwanza kwa kuwa anafuatilia paspoti yake nchini Zambia huku mshindani wake Haruna Niyonzima akiendelea kukiwasha ndani ya Yanga ila kwa sasa inaelezwa kuwa anaumwa Malaria.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic